NIMEAMINI NJIA ZA MUNGU HAZICHUNGUZIKI

PETER MICHAEL MABULA

BIBLIA TAKATIFU

Ndugu zangu nawasalimu katika jina la YESU KRISTO. Napenda kuwatia moyo ndugu zangu ya kwamba MUNGU anatenda miujiza kwa njia yeyote na hazuiliwi na chochote. Kwa muda sasa nimekuwa napost neno la MUNGU au ujumbe wenye mafundisho ya Biblia ili watu wengine wabarikiwe,wafundishwe,waonywe na waongezeke kiimani na namshukuru sana MUNGU hilo agizo lake nimekuwa nalifanya na ajabu ambayo imepelekea hadi kuandika ujumbe huu ni shuhuda za watu 7 ambao wameniambia wamepata uponyaji kwa kusoma tu post za neno la MUNGU. kwa hilo nimemshangaa sana MUNGU na nimekubali kwamba ''njia zake hazichunguziki'' kama Biblia inavyosema. na yote haya ametenda kwa upendo wake hivyo sifa,utukufu,heshima,adhama na enzi yote ni yake JEHOVAH MUNGU wetu. ninachokuomba ndugu endelea tu kupost ujumbe wa neno la MUNGU na kile ambacho ROHO WA MUNGU anaweka ndani yako wewe kama mtoto wake uliyeokolewa kwa neema na YESU KRISTO. washuhudie watu kuhusu YESU kwani hakuna uzima kwingine nje na yeye. Na kupingwa kupo ila usikate tamaa maana mfano mimi wengi sana wameni-block ambao hawataki ujumbe wa neno na wengi wao ni wakristo majina ila tu hawataki kukemewa dhambi zao na wengine wamenitukana sana kwenye wall yangu au inbox ila namshukuru sana MUNGU kwani matusi yalipozidi ndipo ujasiri zaidi uliongezeka kwangu na kama watu wakini-block au kuni-unfriend ndivyo wengi zaidi walitaka tuwe marafiki kwa hilo
namshukuru sana MUNGU. Wote tunahijatiana yaani nionye ninapokosea na na wewe kubali kuonya au kufundishwa unapokosea au unapokwenda sivyo maana hata Biblia inasema ''mfundiishane,muonyane na mwombeane'' na yote yatendeke kwa upole na bila chuki yeyote.hivyo tumia nafasi yako ndugu kupost neno la MUNGU na kufariji wengine.Ni hayo tu MUNGU awabariki sana wote watakaosoma ujumbe huu na naamini MUNGU ameshatenda miujiza mingi kwa wengine kupitia wewe hata kama hujafanikiwa kujua hilo au kuona ila amini kwani anayeponya sio wewe ni MUNGU hivyo kujua au kutokujua isikushughurishe ila songa mbele na YESU KRISTO na wasaidie na wengine waijue hii kweli ya YESU na hiyo kweli iwaweke huru.

By Peter Michael Mabula
Maisha ya ushindi.
0714252292
PETER M MABULA

Comments