{Ningeomba uniandikie sara ambayo ntaitumia wakati wa usiku na asubuh kazi njema} NI SWALI LILILOULIZWA NA NDUGU MMOJA KATIKA PAGE YETU YA MAISHA YA USHINDI KATIKA FACEBOOK NA HAYA NDIO MAJIBU ALIYOJIBIWA AMBAYO YATASAIDIA NA WENGINE WANAOOMBA MAOMBI YA KUKARIRI}
asante
sana kaka kwa kile ulichoniomba nikuandikie sara ya kuomba usiku au
mchana.Kaka maombi halisi ambayo MUNGU anataka si yale ya kukariri bali
MUNGU anataka uombe kana kwamba unamwomba rafiki yako ila katika maombi
yako muda wote nakuomba zingatia yafuatayo; 1.katika maombi yako anza na
kumshukuru MUNGU kwa ulinzi wake kwako 2.tubu kwa MUNGU hata kama hujui
kama umetenda dhambi yeyote maana sisi wanadamu wakati mwingine huwa
tunatenda dhambi pasipo kujua hivyo tubu kwanza maana Biblia inasema
maombi ya mtu mwenye dhambi MUNGU hayajibu hivyo kama unataka MUNGU
ajibu maombi lazima utubu kwanza 3.omba chochote kwa MUNGU na yeye
atakujibu 4.baada ya maombi yako yoyote shukuru kwa MUNGU kwani hata huo
muda wa kuomba MUNGU ndio aliyekupa. ukiomba kwa kuzingatia hivyo
vipengere MUNGU lazima atakujibu maombi yako lakini lazima licha ya
kufanya yote hayo lazima uwe umeshampa YESU maisha yako kwanza. kaka
zingatia tu hivyo vipengere 4 yaani kushukuru,kutubu ,kupeleka mahitaji
yako kwa MUNGU na kushukuru. pia kumbuka maombi yako yote omba katika
jina la YESU na hitimisha katika jina la YESU. ni hayo tu kaka ubarikiwe
sana na nakutakia siku njema na ukizingatia hayo lazima utaona matokeo
na lazima pia uombe kwa imani pia soma mistari hii katika Biblia ili
ikusaidie katika maombi yako; YOHANA 14:14, ZABURI 136:1-26,WAEBRANIA
11:1 NA WAEBRANIA 11:6.AM
HAKUNA
ATAKAYEMWONA MUNGU PASIPO UTAKATIFU HIVYO HATA KWA MAOMBI YAKO
HAKIKISHA UNAOMBA UKIWA MTAKATIFU KWANI MUNGU NI UTAKATIFU![]()
|
Comments