Posted by
Peter Mabula
- Get link
 - X
 - Other Apps
 
![]()  | 
| MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE | 
Mimi na mke wangu na familia yetu yote- yaani watoto ma wajukuu, tunakutakia siku njema ya krismasi.
 Ujumbe nilionao kwako ni Mathayo 2:1-23. Ndani ya ujumbe huu napenda kukuambia mambo mawili makubwa
 Jambo la Kwanza,
 Yesu Kristo alipozaliwa Bethelehemu, si kila mtu alifurahi. Biblia 
inasema ya kuwa kuzaliwa kwa Yesu kuliposikika: " Mfalme 
Herode....alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye"(Mathayo 2:3). Kwa 
hiyo, hata wewe usishangae unapoona si kila mtu anafurahi juu ya kuokoka
 kwako. Si kila mtu atafurahi atakapoona Yesu anazaa kitu moyoni mwako. 
Na pia usitegemee kuona kila mtu anayekuona unadumu katika Kristo 
atakufurahia
 Jambo la Pili,
 Kama vile Mungu alivyomsaidia na 
kumlinda Yesu alipozaliwa asiuwawe na wale waliochukia kuzaliwa 
kwake,uwe na uhakika Mungu huyu atakilinda kilicho cha Yesu katika 
maisha yako, kisiuwawe na wanaokichukia.
 Naamini ujumbe huu utakutia moyo katika siku hii muhimu.BY MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE


- Get link
 - X
 - Other Apps
 

Comments