SHETANI AMEPUMBAZA WATU AKILI KATIKA ENEO HILI{KINGA/TAHADHARI}

Nimekuja kugundua kwamba watu wengi hasa watanzania wamekuwa wakiteswa na magonjwa sana na wamekuwa wakipoteza fedha zao nyingi kutibu magonjwa, kutokana na shetani kuwapumbaza katika eneo moja tu ..(kinga/ tahadhari). Wengi hawafuatilii afya zao, hawajali na wala hawachukui tahadhari za kujikinga na magonjwa hayo. Wakianza kuumwa wanaanza kulalamika na kuona kama Mungu amewaacha... wengine wamejikuta wanapatwa na magonjwa yasiyotibika hospital kama kisukari, ukimwi, cancer nk.

Mwaka 2013 tuanze kampeni pamoja katika kuharibu vyanzo vya magonjwa haya kwa kuchukua tahadhari mapema kabla ya kuyapata. Si mpango wa Mungu wewe uugue...! Ni mpango kamili wa shetani ndio maana amefunga fahamu za wengi katika hili kiasi kwamba hawaelewi mpaka wakishatumbukia katika magonjwa haya ndio wanaanza kufunguka na kuanza kujuta wakisema laiti tungejua. Nakupa mfano 1. Mtu yuko tayari kunywa soda hata 4 kwa siku au hata bia 10 lakini kununua embe au chungwa moja akala ni taabu, au kunywa maji kwake eti yanamchefua....!

"YESU alimaliza magonjwa yote pale msalabani.. ni kweli.. ila huwezi kwenda kukaa sehemu yenye mbu kwa makusudi, wakung'ate sana alafu uache kupata malaria, au huwezi kula kwa ulafi tena vyakula vyenye cholesterol kwa muda mrefu uache kupata pressure na mengine.


Comments