UNAWAJUA WA KWANZA KUINGIA JEHANAMU?

SOMA KWA MAKINI UJUMBE HUU NA UKUSAIDIE WEWE NA UWASAIDIE NA WENGINE NA BIBLIA INASEMA ''Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa linalowaka moto wa kiberiti, walimo yule mnyama na yule nabii wa uongo, nao watateswa mchana na usiku, milele na milele.''{Ufunuo 20:10} Maana hawa ni utatu wa shetani na hata waumini wao lazima waupinge UTATU MTAKATIFU WA MUNGU, Pia ndugu kumbuka joka ndiye shetani mwenyewe, mnyama ni msaidizi wa sh
etani ambaye dini nyingi sana wanamuabudu na huyu mnyama ana pembe nyingi yaani maana yake ni dini nyingi sana au matawi yake ambayo yote yanamwabudu shetani bila kujua na katika hizo pembe au dini kila sehemu kajigeuza na kuonekana tofauti na dini nyingine kumbe zote ni dini za shetani na huyo nabii wa uongo ni yule kinara wa manabii wa uongo ambaye unamfahamu na wote hawa adui yao mkubwa ni BWANA YESU KRISTO aliye njia pekee ya uzima wa milele{yohana 14:6}. harafu ndugu sikutishi wala kukuchanganya akili lakini nataka ufahamu ukweli maana unakuta wazazi wafuga majini lakini haohao ndio wa kwanza kuchapa watoto wao ili waende wakajifunze dini hiyo ni ujinga sana na ndio maana YESU KRISTO alisema kipofu hawezi kuongoza kipofu mwenzake. wewe uko kwenye dini na nabii wa kwenye kitabu chako anakuambia kwamba hata yeye hajui atafanywa nini siku ya mwisho sasa hiyo ni dini au balaa.ndugu kama unataka uzima wa milele basi mpe YESU KRISTO maisha yako pia usitumie visanamu vyovyote kumwabudu MUNGU viwe vya kuvaa shingoni au hata vya kuwekwa kwenye nyumba za ibada kwani hayo ni machukizo makuu kwa MUNGU. MWISHO KUMBUKA KUWA HIZI NI NYAKATI ZA MWISHO NA WAKATI WA KUOKOKA NI SASA HIVYO CHUKUA HATUA, NAKUFUNIKA KWA DAMU YA YESU KRISTO NA MUNGU WANGU AKUBARIKI SANA KATIKA JINA LA YESU KRISTO AMEN. pia ujumbe huu nakuomba uwafahamishe na wengine ili waujue ukweli wa JEHOVAH MUNGU ambaye ndiye MUNGU pekee wa kweli na ambaye wewe na mimi kama tunautaka uzima wa milele ni lazima tumpe BWANA YESU maisha yetu zaburi 83:18{Wajue ya kuwa wewe uitwaye jina lako YEHOVA ndiwe peke yako uliye juu ya nchi yote}, barikiwa sana

Comments