Ndugu katika BWANA YESU shalom. MUNGU akubariki sana popote ulipo na leo nakuletea ujumbe kuhusu ndoto.Kuna watu wanapinga kuhusu uhakika wa ndoto,lakini ukweli ni
kwamba Mungu hutumia pia njia ya ndoto kumpelekea mtu ujumbe Mathayo
2;11-15 inayozungumzia Mamajusi pamoja na Yusuphu ambao walipewa ujumbe
kupitia ndoto.
kuna kasumba ya kwamba mtu anaweza kuota kutokana
na kile alichokuwa akikiwaza siku nzima ama akikifanya lakini ukweli wa
hayo ni kidogo sana kwani ni mstari mmoja tu kwenye biblia ndio
unaotofautiana na ndoto Muhubiri 5;3 pia soma mstari wa 7,cha msingi ni kutafakari ndoto uliyoota kama ni mbaya hiyo ni kengele
ya hatari unatakiwa uingie kwenye maombi kukemea ili isitimie,
'' kuna wakati kuna watu wanaota wanakimbizwa na mtu ameshika silaha ama
kitu fulani anataka kupigwa nacho,ama wanaota wako katikati ya msitu
wanachofanya wanajitingisha ili watoke kwenye hiyo ndoto wakifanikiwa
wanahema na kuhema ooh asante YESU nilikuwa naota, hiyo haitoshi ni
kwamba umekatisha tu hiyo ndoto kuna siku itakurudia tena dawa yake ni
kuomba ulinzi kwa Mungu yawezekana ni kweli kuna mtu anafatilia maisha
yako kwa hila''.
unapoota ndoto kama yakukimbizwa,au mtu anataka kukuua unatakiwa
ujihoji yawezekana ni ishara ya kukuonyesha kwamba utengeneze mambo
yako haujakaa sawa, pia tambua kuwa MUNGU amezungumza na watumishi wake kupitia ndoto kama
1Wafalme 3;5-10, Ayubu 7;14, Daniel 2;1,Daniel 7;1,.
Aidha yawezekana unaota ndoto moja zaidi ya mara
mbili,yawezekana ya kufanya kitu fulani ambacho kwa mtazamo na hali
uliyonayo unaweza kusema haitaweza kutokea,amesema hiyo ni ishara ya
kiroho kwamba hicho kitu kitakuja kutokea cha kufanaya ni kuomba pia
kuwa na kawaida ya kuandika kile unachoota na na soma pia maandiko kutoka
Hesabu 12;6 pamoja na Ayubu 7;14
Sababu nyingine nyingine ni kwamba asili ya ndoto ni lugha ya roho, ni ujumbe wa
Mungu kuhusiana na maisha yako Ayubu 20;8, akasema kama unalala pasipo
kuuliza ulinzi wa Mungu na pia kumuomba Mungu akupe ndoto nzuri, shetani
atanyemelea nafasi hiyo na kufanya kazi yake,akatolea mfano wa Yusuphu
aliyeota wazazi wake na ndugu zake kumsujudia hali ambayo waliipinga
sana na ndugu zake kuamua kumuuza kwa wa Misri alipofika kwa Potifa mke
wa potifa akataka wafanye dhambi ambayo Yusuphu aliikwepa lakini
akajikuta gerezani huko nako aliwatafsiri ndoto wafungwa wenzake na
ikatokea kama alivyosema kisha kutafsiri ndoto ya Farao iliyokua kumpa
uwaziri mkuu kilichotokea ndugu zake walikuja kule kwasababu ya shida ya
chakula, yakatimia walimsujudia kama alivyoota, kwahiyo kama una ndoto
yoyote maishani omba fanya bidii itimie. na katika kila ndoto husika na mambo haya kama ni ya mbaya omba maombi yenye nguvu kuzuia katika jina la YESU na kama ni ndoto ya kimungu mshukuru MUNGU kwa maombi na pia kama umeota kibinadamu kwa sababu ya kuliwazia sana jambo hilo basi omba MUNGU ili lile alitakalo yeye ndio litimie. na Ndugu kumbuka kwamba mambo yote huanzia kwanza katika ulimwengu wa roho hivyo hata kama ni ajari hupangwa kwanza katika ulimwengu wa roho ndipo inakuja kutokea hivyo ili mambo mabaya ambayo shetani ameshapanga ili yasije kwetu lazima tufunje kwa jina la YESU na mambo hayo wakati mwingine unaweza kuonyesha kwa njia ya ndoto hivyo kemea kwa jina la YESU pia hata mambo mazuri ambayo MUNGU anapanga juu yetu pia wakati mwingine yanaweza kufunuliwa kwetu kwa njia ya ndoto hivyo mshukuru MUNGU kwa maombi.Na mambo haya unaweza ukaota leo na jambo hilohilo likaja likatokea baada ya yaku mbili mbele au wiki moja,mwezi, mwaka au miaka 3 au zaidi hivyo kudhibiti mapema ni jambo jema sana. MUNGU akubariki sana.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

![]() |
MAOMBI NI ULINZI TOSHA NA TUKIMWOMBA MUNGU ULINZI ILI ADUI ASIFANIKIWE MUNGU HUJIBU NA KUTUZINGIRA![]() |
Comments