WACHAWI WALINIPINGA NISIOKOKE KWA KUNITUMIA KUNGURU WANITAFUNE

SHIJA WA TATU KUTOKA KUSHOTO AKIWA NA RAFIKI ZAKE HUKO MKOANI MBEYA
BWANA YESU asifiwe. Naitwa shija michael nina miaka 28 ni mwenyeji wa mkoa wa mbeya  napenda nishuhudie kile ambacho MUNGU amefanya maishani mwangu. kwa muda mwingi sana niliteseka na kuteswa na nguvu za giza kuna rafiki yangu kazini kila muda alikuwa ananiambia niokoke ili niache ngono,pombe na sigara ambazo zilikua zimenitawala kwa muda mrefu sana lakini baya zaidi ni majini na uchawi ambao nikuwa nauona maana MUNGU alikuwa amenifumbua na nilikuwa naona muda mwingi tu usiku wakicheza nje ya nyumba na wakati mwingine wakija ndani na kuanza kushtua watu ili waone ni nani anawaona kwa muda huo wote nilijikausha ili wasidhani nawaona baada ya miaka kadhaa mwaka 2011 waligundua kwamba nawaona kwani siku moja usiku nikiwa chumbani kwangu walikuja na nilishtuka sana hadi wakajua na baada ya hapo walisema lazima waniue kwani nina kipaji cha ajabu na wakikubali nimpe YESU maisha nitakuwa hatari kubwa sana kwao kwani waliookoka kwa kumaanisha huwateza sana wachawi kwani wana nguvu na mamlaka kupita zote . Kesho yake nikiwa kazini nilimwambia yule kaka mtumishi ambaye huniambia habari za kuokoka kwamba ipo siku nitaokoka na tena sio siku nyingi nitachukua hatua hiyo ila nilimficha yaliyotokea kumbe sikujua kwamba nilikuwa nafuatiliwa na wale wachawi na majini usiku ule nililala kazini sio kule nilikopanga na usiku ule niliugua ghafla nikajua nakufa maana niliteseka kuanzia saa 3 usiku hadi saa 8 usiku na nilishidwa hata kuongea na hata kusema neno lolote kwani nikiongea sauti haitoki na nikiongeza kusema kwa sauti zaidi ndivyo sauti inapungua zaidi na nilijua mwisho wangu umefika nikaanza kutubu kimoyomoyo na kumwambia BWANA YESU aniokoe na mimi ili nisiende motoni baada ya kuomba kwa muda nilimwita rafiki wa kitanda cha jirani maana sisi ni askari ili akamwite yule mtumishi aje aniongoze sala ya toba maana nakufa na nilikua nimeshaikubali hiyo hali ya kufa  yule mtumishi akaitwa akaja akaniongoza sala ya toba akiniambia nitamke hivi ''EE BWANA YESU, NAKUJA MBELE ZAKO, MIMI NI MWENYE DHAMBI, LAKINI LEO NAGEUKA NA KUTUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAZOKUMBUKA NA NISIZOKUMBUKA, MAANA LEO NAMEOKOKA, FUTA JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, NA ULIANDIKE JINA LANGU KWENYE KITABU CHA UZIMA, MAANA LEO NIMEOKOKA, NIZINGILE KWA DAMU YAKO ,NA ULINZI WAKO, KATIKA JINA LA YESU KRISTO, AMEN.'' maneno hayo nayakumbuka sana hadi leo na baada ya kuniongoza kwa sala hiyo alianza kuniombea na kuna vitu nilihisi na kusikia vinaondoka mwilini mwangu na baada ya hapo nilijiona mwepesi na nimepata nafuu nikajua BWANA YESU ananipenda sana na amenisaidia. Usiku ule ule nikamwahidi huyu kaka mtumishi kwamba kesho tutaenda wote kanisa kwao na kesho baada ya muda wa kazi saa 8:30 mchana nilimwambia anisubiri niende kwanza chumbani kwangu nilikokua nimepanga nikabadirishe nguo na kurudi hapo ndipo nilipatwa na jambo la ajabu ambalo kwa hilo hadi nimeamua kushuhudia nilichukua baiskeli yangu na kuanza kuendesha na nilipotoka tu nje ya kambi kundi kubwa la ndege wakubwa yaani mwewe na kunguru walianza kunifukuza na nikadhani labda kuna kitu mgongoni kwangu ambacho wanataka kuchukua na nikasimama nikavua tshirt ili nikague nikakuta hakuna chochote nikavaa haraka haraka huku wakinizonga wanidonoe mwilini mwangu nikaongeza mwendo wa baiskeli yaani nikaanza kuendesha baiskeli kama sina akili timamu yaani kwa spidi ya ajabu na wale kunguru hawakuniacha bali waliongeza spidi hata sikuweza kuwaacha na hadi wengine wakawa wananivuka na kugeuka ili waniume machoni ila nakwepa na ajabu ni kwamba hao ndege waliongezeka na kuwa kundi kubwa sana baadae kidogo nikiwa nakaribia nyumbani nilisikia sauti ikisema na unabahati umeokoka mapema tulikua tumekuja kukuua bahati yako ni huo ukuta wa moto aliokuzingira huyo YESU lakini kwa hofu sikuwaamni nilijua tu wanataka kuniua na niliongeza sana spidi ya baiskeli hadi mwisho  na nilifika nyumbani ghafla na kuingia ndani baiskeli nikiitupa mlangoni nikakumbuka kwamba licha ya kuombewa usiku na kupona lakini asubuhi nilivuta sigara na kunywa pombe kidogo kwani ilikuwa ngumu kuacha ghafla ila nilimficha yule mtumishi maana angenishangaa na MUNGU ni utakatifu hivyo hata kunilindwa vile wasiniue ilikuwa ni neema yake tu kwani nilikuwa nimeshamkosea tayari licha ya ktubu kwa uchungu usiku wa jana yake. nilikaa mule chumbani kama saa nzima na muda huo wote nilikua natubu kwa MUNGU  na kumwomba BWANA YESU aliandike tena jina langu kwenye kitabu cha uzima na baada ya hapo  nilihisi amani moyoni na nikafungua dirisha kuchungulia kama wale ndege bado wapo sikuwaona na nikatoka nje sikuwaona nilichofanya nilimwambia kijana mmoja wa jirani na ninapokaa anisindikize kambini na alikubali tukaondoka ila yye hakujua kwamba nataka awe msaada wangu kama wakija tena wale kunguru na mwewe tuliondoka na tukafika salama nikamkuta yule mtumishi bado akinisubiri tukaondoka na kwenda kanisani akamweleza mchungaji nikaombewa zaidi na kuwa huru. MUNGU ni mwema sana na ameniokoa na kunishindia na mabaya haya yote sifa na utukufu namrudishia yeye aliye pekee mweza yote yote kiukweli hakuna rafiki muhimu na sahihi zaidi ya YESU KRISTO. 
MUNGU na akubariki sana AMEN.

Comments