WEMA UTALIPWA KWA WEMA NA UBAYA UTALIPWA KWA UBAYA

Siku moja, kijana maskini ambaye alikuwa akiuza bidhaa zake mtaa kwa mtaa ili mradi ajipatie ada ya wenda shule. Baada ya kuuza bidhaa zake huku akitembeza juani kwa muda mrefu sana alijihisi njaa kali tumboni mwake. Siku hiyo ilikuwa mbaya sana kwake kwani hakuweza kuuza kabisa.

Akili ilimjia a
ende nyumba ya jirani yake kugonga japo aombe chakula hata kama ni kidogo ili mradi tumbo lake lipate chochote. Alipofika nyumba ya hapo jirani yake, aligonga mlango na kisha akafunguliwa na msichana mrembo hali iliyomfanya kijana huyu apoteze ujasiri.

Yule kijana alishindwa kabisa kuomba chakula hali iliyomfanya ajikut anaomba maji ya kunywa badala ya chakula kama alivyodhamiria.
Ndani ya muda mchache yule dada aliingia ndani kisha akatoka na kikombe kilichojaa maziwa kisha akampatia yule kijana. Akanywa hivyo polepole, na kisha akauliza,
“kiasi gani nadaiwa..? "

“Hudaiwi chochote kwani nimekusaidia kama msaada na kwa jinsi nilivyokuona umechoka.. na hata hivyo Mama ametufundisha kamwe kukubali kulipa kwa wema. " Alisema yule msichana mrembo.
... Ahsante ninakushukuru sana.."

Kijana huyo aliokuwa anatambulika kama Howard Kelly alivyomaliza kunywa yale maziwa alishukuru nakuendelea na biashara yake ya kutembeza bidhaa zake mtaa kwa mtaa na alijipa moyo na nguvu za kijasiri nakuahidi kamwe hatokuja kumdharau mwanamke na aliapa kujitoa kwa kila mali hapo baadaye.

Baada ya miaka saba kupita, Mwanamke mmoja alikuwa mahtuti. Madaktari walihangaika sana kumhudumia kwa kila hali na mali lakini hali yake ikawa ni mbaya zaidi. Hatimaye jopo la madaktari wakaamua wampeleke mji mwingine kwa kwa wataalamu zaidi kwani ugonjwa wake ulikuwa unatibiwa na madaktari bingwa wachache sana.

Dr Kelly Howard alikuwa ni mmoja wa madaktari bingwa wa uginjwa aliokuwa akiiumwa huyo msichana. Ilibidi dr. Kelly Howard amtibu mgonjwa huyo. Alipofika wodini alishangazwa kumuona msichana mrembo na sura yake haikuwa ngeni katika mboni ya macho yake. Alichokifanya Dr. Kelly Howard alitoka mule wodini nakuingia chumba cha madaktari kisha akavaa nguo zile za kufanyia operesheni yeye pamoja na wenzake sita na kuingia kwenye chumba cha operesheni nakuanza kumfanyia huyo msichana.

Baada ya Masaa matatu ya operesheni uso wa Dr. Kelly Howard ulikuwa na fuaha baada ya kufanikiwa kuokoa maisha ya yule msichana na sasa. Alichokifanya Dr. Kelly Howard ni kuchukua kitabu chake cha hospitali cha bili kisha akaandika maneno machache akawapa manesi wampelekee yule msichana wodini.
Kile kikaratasi kilipomfikia yule msichana alishtuka na kuogopa kufungua kwa maana aliposikia kinatoka kwa dokta aliyemfanyia operesheni alijua wazi hajapona na huenda tatizo limekuwa kubwa zaidi. Alijipa moyo konde kisha akakifungua na kuanza kukisoma..
"Nimelipa wema kukufanyia operesheni bure kama ulivyonipa kikombe cha maziwa hapo zamani.." (saini) Dr Howard Kelly.
Machozi ya furaha na msisimko wa mwili uliongezeka kwa yule msichana baada ya kujua kuwa kumbe aliyemfanyia operesheni ni yule aliyowahi kumsaidia kikombe cha maziwa hapo zamani. Alichukuwa kile kikaratasi akakibusu kisha akakilaza kifuani mwake huku machozi ya furaha yakiendelea kumbubujika huku akiongea peke yake:
"Asante, Mungu, kwamba upendo wako unaenea kupitia nyoyo za binadamu na mikono.."

::Eneza ujumbe huu kwa ku LIKE & ku Share kwa watu wengi zaidi ili waelimike kupitia ukweli huu..'

Comments