WEWE NYOKA ONDOKA, USINIUDHI WAKATI MIMI NAONGEA NA BWANA YESU

EDMUND JOHN

Edmund John  ni mwanzilishi wa Huduma ya uinjilisti na maombi nyumba kwa nyumba(HUMANN) Iliyopo buguruni Malapa.

MAJARIBU YA NYOKA.
Edmund alikuwa ana desturi ya kufunga kila ijumaa,sasa sikuhiyo alifunga na akiwa amefunga alipendelea sana kwenda sehemu yenye utulivu,na sehemu yenyewe ilikuwa buguruni kipindi hicho kulikuwa ni kichaka.alikaa huka akisali na kutafakari mpaka saa tisa adhuhuri.Alipokuwa katika matafakari yake alimwona nyoka mkubwa sana akitambaa mbele yake kuelekea upande wake wa kulia.Edmund alifikiri kuwa madhali wakati ule wa jua kali nyoka labda anatafuta mahali penye kivuli ili ajihifadì..basi Edmund hakushughulika na yule nyoka,akaendelea kusali.
Kumbe,yule nyoka hakwenda mbali,alikuwa mezunguka na kujiinua karibu na Edmund.Baada ya muda Edmund alihisi kuwa kuna kitu au mtu amesimama karibu naye upande wa kulia.Alifungua macho ili kuangalia,akamwona yule nyoka amejisimamisha karibu na sikio lake huku akitoa ulimi wake.Edmund alifumba macho akaendelea kusali.kisha akafumbua macho yake tena akamwona bado hajaöndoka.(dalili ziliönyesha yule nyoka alitaka chakula).
Sababu ya imani kubwa aliyokuwa nayo hakuwogopa yule nyoka.Pale pale yalimjia mawazo ya ujasiri kumpa amri.Edmund akaamuru,"Wewe nyoka,ondoka.usiniudhi wakati mimi naongea na Bwana Yesu."mara yule nyoka akaanguka chini,akatambaa akaenda zake,wala hakuonekana tena.
UMEJIFUNZA NINI?

Comments