YESU KANIPONYA UVIMBE TUMBONI ULIONISUMBUA MIAKA MIWILI

MAMA NASHONI BAADA YA KUPONA NA NI MUDA ANATOKA KWENYE MKESHA WA CHRISTMAS TAREHE 24 DEC 2012
       Naitwa jane au jina maarufu naitwa mama Nashoni  ninaishi kawe jijini Dar es slaama na nimekuwa nasumbuliwa sana na uvimbe tumboni mwangu kwa muda wa miaka 2 na nimeshakwenda hospital lakini gharama za upasuaji zikawa ni kubwa sana na mimi pamoja na mme wangu hatukuwa na pesa hiyo ya matibabu na baada ya kushindwa kutibiwa nilikaa tu maana nilikata tamaa sana na hadi kuwa nahisi kufakufa lakini namshangaa sana MUNGU kwani jumatatu nilikwenda kwenye mkesha kanisani kwetu PAG KAWE na nilienda baada ya muda mwingi sana kupita sijaenda kanisani kwa sababu ya huu uvimbe lakini wakati wa maombi muda kama wa saa 7 usiku wakati maombi yanaendelea  mchungaji akatuambia tutulie kuna jambo anataka kutueleza  na tukatulia wote na akasema kama kuna mtu anauvimbe au anaumwa chochote aje mbele aombewe na atapona muda huohuo nilikwenda huku nimekata tamaa lakini kwa muda kama dakika moja tu ule uvimbe uliyeyuka ghafla huku nahisi ni kama huna anayeuondoa na kuutupa nje na nikashangaa kwa uponyaji huo. nikasema kweli YESU ni Alpha na Omega maana jambo ambalo limenisumbua mika miwili hadi nimekata tamaa ya kuisha lakini lilipotajwa jina lake nikapokea uponyaji ndani ya dakika moja . Namshukuru MUNGU kwa uzima mpya alionipa na sina cha kumlipa kwa alichotenda maana sikioni hata kimoja cha kumlipa ukilinganisha kile amenitendea. tena bure kabisa bila hata kutumia hata shiling 1 sifa na utukufu namrudishia yeye MUNGU na furaha yangu iliyopotea muda mwingi imerudishwa na YESU kwa muda wa dakika moja.MUNGU awabariki sana na muujiza huu nimeupata kanisani P A G KAWE AU kwa kifupi KPC karibu na kambi ya jeshi lugalo kwa mchungaji ELLY BRIGHTON BOTO MUNGU ambariki sana mtumishi wake huyu.                                                                                            

Comments