DHAMBI YA KIBURI NI MBAYA SANA





Kiburi ni kinyume cha unyenyekevu, ni machukizo makubwa sana mbele za Bwana Mithali 16:5, lazima tuchukie kila namna ya majivuno na kiburi, yeye tunayemfahamu kwa jina leo shetani hakuwa hivyo tangu mwanzo, alijiona kuwa sawa na Mungu, alijiona ni zaidi ya Mungu na hatimaye akatupwa hata nchi. Isaya 14:12-15. Mwenye kiburi hatakosa adhabu ndivyo ilivyokuwa kwa shetani, sisi nasi kama tutaruhusu kiburi kiwe katika maisha yetu tutajiunga na adhabu ya shetani. Dhambi ya kiburi inakuwa ndani sana ya moyo wa mtu, Marko 7:21-23...kiburi na upumbavu haya yote yatoka ndani. Mtu mwenye kiburi hana hofu ya Mungu, akisikia Neno haguswi na Neno hilo, anabaki mkavu tu, Isaya 66:2 ….mtu huyu ndiye nitakayemwangalia mtu aliye mnyonge(mnyenyekevu) …..atetemekaye asikiapo Neno langu. Yeremia 23:9. Jaribu kukumbuka ulipookolewa, ulikuwa mnyenyekevu na kuwa tayari kuyatenda Maneno ya BWANA, unajiona unajua yote,
Unakuwa kama shetani ambaye alijiona anajua yote, na sawa na Mungu. Kama hufanyi maombi kama mwanzo, husomi Biblia kama mwanzo, huna hofu ya Mungu kama mwanzo, ujue dhambi ya kiburi tayari imekuvaa. Tunahitaji kumwambia Bwana atusamehe na kuondoa Kiburi ndani mwetu. Mwenye kiburi ni vigumu sana kujiona ana kosa, ni vigumu sana kukiri kosa, lugha ya mwenye kiburini hii=> Ayubu 33:9 mimi ni safi sina makosa, sina hatia wala hapana uovu ndani yangu. Kiburi cha mtu kitamshusha, Mithali 29:23 Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa. Unafanya dhambi na huna uwezo wa kushinda dhambi lakini hutaki kuokoka hicho ni kiburi.
BWANA niepushe na dhambi ya kiburi.

Comments