Posted by
Peter Mabula
- Get link
- X
- Other Apps
wapendwa katika Bwana,kitu ambacho mwanadamu aliumbwa nacho ni nguvu ya
kuamua.namaanisha hivi,unachokiamua aidha mfumo wa maisha yako
unayoishi yatajulisha uko kwa Mungu au gizani.
Kwa watu wa Mungu
huwa tumezungurushiwa uzio/boma{mhubiri 10:8}wigo wa ulinzi ambao
haumruhusu Shetani maishani mwetu.Sasa jambo la kujua ni kwamba,Wigo huo
haukuzuii kutoisikia sauti ya Shetani,utamsikia ila hawezi
kukugusa.Sasa kinachotokea Shetani atatumia kufanya kila njia ili apate
kiupenyo cha ule wigo aingie ndani yako..je wigo huu tunaubomoaje?..ni
kwa kutokuwa mvumilivu,kutosamehe na kuruhusu hasira tena kwa
kusikitisha mtu wa Mungu unakubali kukasirishwa na mtu asiyemjua Mungu.
NOTE:Shetani hutumia watu ambao hawana uzima ndani yao kama agenti wa kukuangusha.kuwa makini.
UHALAKI WA SHETANI KUKUTAWALA.
1.kwa kufanya dhambi za Amali.
amali(kwa hiari yako).yaani unajua unachokifanya i.e ulevi,uzinzi,matusi,uongo n.k.
2.Kwa njia ya ushirikina
3.Kwa kurithi mikoba.unaweza kurithishwa bila kujua,na hii hutokea kama hauna Yesu.
4.Roho ya kutosamehe.huu ni mlango ambao shetani anautumia
sana.Filemoni 1:8-20,filemon mambo yake hayakwenda vizuri sababu
hakumsamehe Onesmo.
5.Majanga mazito.mfano usaliti,kufiwa n.k
6.Maunganiko ya nafsi sio kwa utukufu wa Mungu.
mfano:maagano ya damu,uzinzi(1kor 6:16-18)unakuwa nafsi moja ya uzinzi.
7.Kuathiriwa na tabia mbaya(being adicted)mfano:Ulevi,ulafi wa kula na uongozi na ulev wa picha chafu za ngono..
Mungu atusaidie tusimane imara tusimruhusu shetani.MUNGU awabariki sana.by RAPHAEL MBOGO
![]() | ||
RAPHAEL MBOGO
|
- Get link
- X
- Other Apps
Comments