Posted by
Peter Mabula
- Get link
 - X
 - Other Apps
 
![]()  | 
| GASPER MADUMLA | 
 Ninakukaribisha mpendwa katika tafakari hii.
 Ambayo inakuhusu wewe pia na mimi maana sisi sote tumetokana na wazazi 
wetu wa kimwili,yaani tulizaliwa kwa jinsi ya mwili licha ile jinsi ya 
kiroho,ambayo kwa hiyo sisi si mali ya shetani tena bali ni mali ya 
Mungu Baba wa mbinguni,tena kwa hiyo sisi tunao ukombozi yaani msamaha 
wa dhambi.
 
 Ni ukweli kabisa kwamba twaweza kurithi MAOVU na LAANA kutoka kwa mababa zetu waliopita ENDAPO KAMA MILANGO YAO IKO WAZI.
 
 Labda nikupe mfano mdogo;
 Tazama yale makabila kumi na mawili ya wana wa Israeli,Yale makabila 
yalikuwa na watu ( watoto wa Yakobo kumi na mbili ) ambao leo hii hatuko
 nao kimwili lakini MALANGO yao yalikuwa wazi,na ndio maana kukuwepo na 
muendeleo wa kabila hizo kumi na mbili, HIVYO WOTE WALIKUFA LAKINI 
MALANGO YAO YAKO WAZI
 Soma EZEKIELI 48 :30-35
 
 Hapo 
awali,Wazazi wetu wetu wea kwanza,walipotenda dhambi na kulaaniwa basi 
ilikuwa ni  moja kwa moja zile laana zilikuwa na uwezo wa kutufuta sisi 
na kutuingiza katika hukumu ambayo tulikuwa hatujahusika kwa dhambi 
yoyote ile tena wala hatujui baba zetu walichokifanya.
 Haleluyaaa..
 
 Tunasoma Warumi 5 : 19
 “ Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa 
katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi 
wameingizwa katika hali ya wenye haki. ”
 
 Pia,
 Tunasoma MAOMBOLEZO 5 :7
 “  Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao.  ”
 
 Wazazi hawa walipoasi mbele za Bwana Mungu,ile dhambi ya kuasi ilikuwa 
na upenyo kuweza kuingia kizazi kimoja hadi kingine,endapo kama mlango 
wa dhambi uko wazi.
 Tazama Kaini alivyoambiwa na Bwana Mungu
 “                                          ”
 
 Ona sasa;
 Kaini aliposhindwa KUISHINDA DHAMBI ILIYOKUWA INAMUOTEA MLANGONI akaja 
akamua ndugu yake, nayo ile dhambi ya mauji na roho  ya mauti haikuishia
 hapo maana mlango ulikuwa wazi, ile dhambi na roho ya mauti  ikasimama 
mlangoni,na baada ya kizazi cha tano,ile dhambi inajirudia tena vile 
vile.
 
 Kumbuka ;
 Kizazi cha kwanza cha Kaini kinaanzia kwa 
mwanaye wa kwanza Henoko,kisha kizazi cha pili ni Iradi,kizazi cha tatu 
ni Mehuyaeli,,kizazi cha nne ni Methushaeli,na kizazi cha tano ni 
Lameki.
 
 Tazama namna ya uovu wa baba zao ulivyopita kuanzia kwa babu yao Kaini mpaka kwa Lameki ,
 Tunasoma ;
 Mwanzo 4 : 23
 “  Lameki akawaambia wake zake, Sikieni sauti yangu, Ada na Sila; Enyi 
wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu; Maana nimemwua mtu kwa kunitia 
jeraha; Kijana kwa kunichubua;  ”
 
 Bwana Yesu asifiwe…,Oooh Haleluyaaa……
 Tazama pia namna ya dhambi na uovu ulivyopita kizazi hadi kizazi 
kikianzia kizazi Abramu ( Ibrahimu ) pale kulipotokea njaa kali ya 
kwanza naye akashuka hata Misri
 
 Tunasoma ;
 Mwanzo 12 : 10-13
 
 “  Basi kulikuwa njaa katika nchi ile; Abramu akashuka Misri, akae huko kwa muda maana njaa ilikuwa nzito katika nchi. 
 Ikawa alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, Tazama, najua ya kuwa u mwanamke mzuri wa uso; 
  basi itakuwa, Wamisri watakapokuona watasema, Huyu ni mkewe; kisha wataniua mimi na wewe watakuacha hai. 
  Tafadhali useme, wewe u ndugu yangu, iwe heri kwangu kwa ajili yako, na nafsi yangu iishi kwa ajili yako.  ”
 
 Tazama sasa na kizazi cha pili cha ISAKA
 Mwanzo 26 :7, 
 “  Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni ndugu 
yangu huyu maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije 
wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa maana alikuwa mzuri wa uso.  ”
 
 Pia ;
  Tazama dhambi ile ile ya kusema uongo iliyoanzia kwa IBRAHIMU,ikaenda kwa ISAKA na mwishoe kizazi cha tatu  cha YAKOBO.
  Hapa utaona Yakobo naye  anamdanganya baba yake Isaka ili apate 
mbaraka ambao ulikuwa unastahili aupate kaka yake Esau  ( SOMA ; Mwanzo 
27 :1-27 )
 
 Na ndio maana dhambi hizi bado hata leo zinatutesa 
sana,watu wengi wamekuwa hawavuki kimaendeleo si kwa sababu hawafanyi 
kazi kwa bidii,bali maovu ya baba yao yanatafuna bidii zao.
 
 Mfano ;
 • Utakuta katika famili,watoto wote wanaishia elimu ya darasa la saba tu,au wengine kikomo chao ni elimu ya form four tu. 
 • Utakuta katika familia,babu kafa kwa ugonjwa wa kisukari,baba naye 
kafa kwa kisukari,mtoto naye alishakufa kwa ugonjwa  wa kisukari,Mjukuu 
sasa ndio  anaumwa ugonjwa huo huo wa kisukari,Na ukiuliza watakuambia “
  AAH! HUU NDIO UGONJWA WETU NDUGU ! ” 
 • Au utakuta katika 
familia,Tatizoi la kuoa au kuolewa ni sugu,yaani watoto wote hawaoelewi /
 Kuoa wakijitahidi sana ni kuishi maisha ya UCHUMBA SUGU na kuzaa watoto
 ndani uchumba sugu.
 
 Ila leo ninakuambia hivi Yesu Kristo U hai kukuponya na hizo laana za mababa waliopita,
 NA KWANZA KABISA ACHA TABIA YA  KUSEMA ETI “ UGONJWA HUU NDIO UGONJWA WANGU,! 
 
 YAANI MWENYE HAYO MAGOJWA NI SHETANI PEKEE, UKISEMA NI UGONJWA WAKO 
MAANA UNATENGENEZA UWE WAKO,NA UTAKUWA HIVYO MAANA NI WEWE MWENYEWE 
UMEUUMBA KWA KINYWA CHAKO ”
 
 Lakini napenda kukutangazia wewe  
mpendwa kwamba ipo njia ya kutatua matatizo haya yote ya 
magonjwa,laana,roho za mauti n.k yaani zootee. Njia  ya kuzuia vyote 
hivi ni YESU KRISTO,PEKEE. Nasema YESU KRISTO TUU ndio dactari wa yote 
haya
 
 Yeyote yule atakayempokea Yesu Kristo kuwa Bwana na 
Mwokozi wa maisha yake,na kukaa ndani yake,kwanza kwa KUFANYIWA IBADA 
MAALUM  YA UKOMBOZI hakika mtu huyo hatakuwa tena chini ya laana zote 
hizo.
 
 Kumbuka ipo njia moja tu ya msamaha wa dhambi pindi utubupo nayo ni DAMU YA YESU KRISTO WA NAZARETI .
 Tunasoma ;
 Mathayo 26 : 28
 “  kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. ”
 
 Wito wangu kwako ;
 Sio kila laana  za kurithi kwamba zinatoka kwa kuongozwa sala ya toba pekee,
 kwa njia hiyo laana nyingine hazitoki ngo’ hata kama umeokoka laikini 
utajikuta laana zinakufuatilia,au utakuta maovu haya ya baba zetu 
waliopita yanakufuatilia 
 hivyo baadae unashangaa na kusema “ Mbona mimi nimeokoka,lakini nashindwa kuaacha UZINZI  ? ”
 Bali laana hizi zinatoka pale tu utakapofanyiwa IBADA YA UKOMBOZI kwa damu ya Yesu Kristo tu.
 
- Get link
 - X
 - Other Apps
 

Comments