Posted by
Peter Mabula
- Get link
- X
- Other Apps
![]() |
MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE |
Shalom!!
Je, unajua Yesu jina lake jingine anaitwa nani?
Mzee Yusufu alipokuwa anaelezwa juu ya kuzaliwa ka Yesu na malaika kwa
njia ya ndoto aliambiwa juu ya majina mawili ya mtoto huyo na
kilichobebwa na majina hayo.
Jina la kwanza aliambiwa katika Mathayo
1:21 ya kuwa: "nawe utamwita jina lake Yesu, maana yeye ndiye
atakayewaokoa watu wake na dhambi zao".
Jina la Pili aliambiwa katika Mathayo 1:23 ya kuwa: " Nao watamwita jina lake Imanueli,yaani Mungu pamoja nasi".
Unadaka hili moyoni mwako? Ndani ya jina la Yesu kuna kukombolewa toka
dhambini. Je kuna dhambi inakusumbua,liitie jina la Yesu uone jinsi
nguvu za Mungu toka ndani ya jina hili zitakavyokusaidia.
Unajisikia
mpweke?Unajisikia kuchukiwa?Unajisikia kukataliwa?kumbuka ndani ya jina
la Yesu kuna nguvu za Imanueli, yaani uwepo wa Mungu ukijifunua kwako
na kwa upande wako. Daka na hili pia moyoni mwako!
Mungu awatunze na kuwabariki.By MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE
- Get link
- X
- Other Apps
Comments