![]() |
MACJAY ZION |
1YOH 1:5-7 "Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake,na kuihubiri kwenu,ya kwamba Mungu ni Nuru,wala giza lolote hamna ndani yake,Tukisema ya kwamba twashirikiana naye,tena tukienenda gizani,twasema uongo,wala hatuifanyi iliyo kweli,bali tukienenda Nuruni,kama yeye alivyo katika Nuru,twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Yesu,mwana wake,yatusafisha dhambi yote" Ndugu yangu mpendwa hauwezi kufanikiwa bila kusamehe,hauwezi ukaponywa bila kupokea na kusamehe rafiki na jamaa zako kwani hata Mungu husamehe kwanza na ndipo kukuponya Zaburi 103:3 "Akusamehe maovu yako yote{DHAMBI ZAKO ZOTE} na kisha akuponya magonjwa yako yote," haijalishi unaumwa nini Yesu kristo huponya,haijalishi vipimo vimesema nin,Yesu amesema ndiyo katika hali unayopitia yeye anakwenda kukuinua ,tazama amesema atafanya njia pasipo kuwa na njia,Amini Mungu amekuinua,amini amekuponya,amekubariki pale unapokwenda kusamehe Mungu aweke mkono wake katika Jina la Yesu kristo aliye hai. MUNGU awabariki sana. B y Macjay Zion

Comments