KWANINI MTU ANAWEZA KUOMBA JAMBO KWA MUNGU NA ASIJIBIWE

WAUMINI WAKIFANYA MAOMBI KANISANI





Katika Yoh14:13 Bwana Yesu anatuahidi kwamba '' Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu,hilo nitafanya,....'
sasa inakuwaje unapiga magoti sana ukifunga na kusali ila Bwana Yesu hatimizi ahadi yake kwako kwa kukupatia lile umuombalo?.

Bwana Yesu asifiwe ndugu zangu mnaonitembelea hapa.

well...ni kweli Bwana Yesu alisema tuombe lolote atatupatia ila mpendwa kuna wakati tunaweza kuomba jambo tusipatiwe...sio kama mungu hasikii maombi hayo...hapana...kuna sababu nyingi za kwanini Mungu anaweza asijibu maombi.

Wakati mwingine ombi linaweza lisijibiwe sababu UNAJARIBIWA ila ukisimama katika imani ipo siku utajibiwa...mfano mzuri ni Sara...Sara hakukata tamaa mwishowe akapewa mtoto akiwa keshazeeka...hebu jiulize ingekua ni wewe ungeweza  kuendelea kumtumainia Mungu au ungekimbilia kwa kalumanzira?.

Vilevile ukisoma katika Yak 4:2-3 utaona kwamba kuna maombi hajibiwi sababu lengo la kinachoombwa halimfurahishi Mungu.Chukulia mfano unamuomba mungu akubariki cheo fulani ambacho kitakusaidia kula rushwa au kujipatia wanawake kirahisi kwa kuwaahidi ajira iwapo watakuhonga ngono.Biblia imeweka wazi kuwa maombi kama haya hayatajibiwa.

Kila tunachomuomba mungu kinatakiwa kiwe na nia safi...Mungu hawezi kukupatia kitu unachomuomba ili ukawakomeshe au unachotaka ili uwanyanyasie jirani zako.

Pia tukumbuke kwamba Mungu ni baba yetu,sisi ni watoto wadogo sana mbele zake,yeye anajua mengi ambayo sisi hatujui hivyo tukimuomba jambo ambalo yeye anaona litatuletea matatizo hatatupatia....sisi tunaweza kumuomba jambo tukidhani ni zuri kumbe yeye kwa macho yake ya kiungu ameona si zuri...kumbuka mtoto wako akikuomba wembe huwezi kumpatia ...hivyo na baba yetu wa mbinguni ni hivyo hivyo.

Comments