Skip to main content
MAANA YA NEEMA YA MUNGU KWETU
 
Nini basi maana ya neema? Watu wengi wamekuwa wakiimba ,”Neema, neema imefunuliwa” na kukariri na kuisema Neema ya Bwana (2 WAKORINTHO 13:14) kama Kasuku huku hawajui wayasemayo. Nini basi maana ya  neema?
- Neema, ni upendeleo wa kuchaguliwa, bila kustahili kutokana na matendo yoyote aliyoyafanya mtu au  sifa aliyonayo mtu.
 
- Neema pia, ni uwezo wa kushinda katika tabia na utumishi wa Mungu 
sawasawa na mapenzi yake, tunaopewa na Mungu bila gharama yoyote au 
nguvuzetu au kufanyia kazi yoyote.
 
- 1.      Upendeleo wa kuchaguliwa bila kustahili- Kutokana na matendo yake, hakuna mwanadamu yeyote mwenye haki mbele za  Mungu (WARUMI 3:20). Tangu kabisa  amekuwa akimhuzunisha Mungu (MWANZO 6:5-7).
 Wakati wa Nuhu, watu waliangamizwa kwa Gharika. Wakati wa Musa, Mungu 
alitaka pia kufuta  kabisa kizazi  cha Wausraeli na kubaki na Musa tu 
kama siyo maombi ya Musa (HESABU 14:11-20). Wakati wote, wanadamu wote wamepotoka na kuoza (WARUMI 3:12). Ni Yesu peke  yake tu ambaye siku zote alifanya yanayompendeza Mungu (YOHANA8:29).Alijaribiwa sawasawa na sisi lakini hakutenda dhambi (WAEBRANIA  4:14-15).
 Yesu huyu anayempendeza Mungu ndiye aliyekufa msalabani na Baraba 
aliyekuwa mhalifu mkubwa akafunguliwa. Kama Baraba alivyofunguliwa 
pamoja na ukosaji wake, kila mwanadamu amefunguliwa, akiamini tu. Mbele 
za Mungu kila mtu amepimwa na kuonekana amepungua (DANIELI 5:27).
 Sasa kwa kuamini tu kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu pale msalabani,
 sisi tunaokolewa. Watu wengi hawaokolewi kwa  sababu  hawajui 
tunaokolewa kwa neema tu kwa njia ya imani peke yake (WAEFESO 2:5).
 Kazi aliyoifanya Yesu msalabani imetupa kuirithi mbingu aliyokwenda  
bila sisi kuifanya. Ni kama ambavyo bondia anavyopigana ulingoni kwa 
shida kubwa na kasha akishinda na kupewa mamilioni ya fedha,  mke wake 
aliyebaki nyumbani bila kupigana naye atakuwa milionea. Hii ndiyo neema.
 
- 2.      Uwezo wa kushinda bila kutumia nguvu zetu- Neema ni uwezo wa kushinda dhambi na kumtumikia Mungu apendavyo. Neema ndiyo inayotufundisha (inayotuwezesha) kukataa ubaya na tama za kidunia na kuishi kwa kiasi na haki na utakatifu (TITO 2:11-12; WAGALATIA 2:8).
 Maisha ya wokovu siyo ya kutumia nguvu zetu au kujitahidi. Uweza wa 
Mungu unatimilika kwetu katika udhaifu wetu yaani kutokuweza kwetu. 
Hatupaswi kujitumainia wenyewe katika kufanya lolote  (2 WAKORINTHO 1:8-9).

 
 
 
 
 
 
 
  
 
 
 
 
 
Comments