MADHARA YA KUZOELEA NENO LA MUNGU

Wana wa Israeli waliangamizwa jangwani kwa sababu walilizoea Neno la Mungu, ingawa kila siku walikuwa wakilisikia (1WAKORINTHO 10:1-5). Wana wa Israeli walifikia mahali pa kudai wapewe mfalme mwanadamu badala ya Mungu aliyekuwa amewachosha, kwasababu walilizoea Neno lake (1SAMWELI 8:4-7), kwa  sababu hiyo, wpte hawakuingia Kaanani isipokuwa watu wawili tu, Kalebu mwana wa Yefune na Yoshua mwana wa Nuni (KUMBUKUMBU LA TORATI 1::35-38). Yuda Iskariote yeye naye yuko motoni leo kwasababu alilizoea Neno la Yesu Kristo ingawa alikuwa naye kila siku. Watu waliookoka siku nyingi au Watendakazi wengi huingia katika mtego wa kulizoea Neno. Tukiisha kulizoea Neno , tujue hatuwezi kuingia Kanaani, yaani mbinguni, bali mahali petu nin motoni. Bwana  atusaidie tusilizoee Neno la Mungu, katika jina la Yesu.
(3).  DALILI ZA KULIZOEA NENO LA MUNGU.
Zipo dalili kadha ambazo tunaweza kuziona kirahisi, kwa watu waliolizoea Neno la Mungu. Tukiziangalia, zitatusaidia kuwa na tahadhari:-
  • Watu waliolizoea Neno la Mungu, huhesabu kwamba Neno linalotoka katika
Kinywa cha Mtumishi   wa Mungu, ni neno lake huyu mwanadamu na wala siyo Neno la Mungu. Watu ambao hawajalizoea Neno la Mungu, huhesabu kwamba neno la ujumbe litokalo katika vinywa vya Watumishi wa Mungu, ni Neno la Mungu mwenyewe (1 WATHESALONIKE 2:13).
  • Watu waliolizoea Neno la Mungu, wanakuwa hawana shauku tena ya
Kuhudhuria  ibada zote. Watu hawa wanachagua kuhudhuria ibada fulanifulani tu na hata wakihudhuria wanaweza wakawa wanazurura nje tu bila kufuatilia Neno. Kwao kuwemo ndani ya nyumba ya Mungu siku zote siyo muhimu tena (LUKA 2:49), tofauti na mwanzoni walipokuwa wachanga kiroho, ambapo waliumia sana kukosa Neni la Mungu siku yoyote.
  • . Watu waliolizoea Neno hujiona wanajua Neno lote na kuona kwamba   maneno yanayofundishwa ni ya wachanga kiroho na siyo ya wale waliookoka siku nyingi. Mtu akijiona anajua Neno, hajajua Neno lolote bado kama impasavyo kujua        (1 WAKORITHO 8;2), ila tu ni kwamba amelizoea.
  • Mtu aliyelizoea Neno, hata akiketi kulisikia Neno, anakuwa mzito sana  kubadilishwa na Neno hilo, na kulitendea kazi kwa sababu roho yake ni ngumu, siyo roho iliyopondeka. Hufikiri ni mjanja kwa jinsi asivyo litendea kazi Neno la Mungu kwa bidii kama wakati wa uchanga wake, kumbe sasa ndiyo amekuwa mpumbavu (MATHAYO 7:24-27).
Bwana atusaidie, ili tusilizoee kamwe Neno la Mungu, na kama tumekwisha kulizoea, tutubu na kumwomba Mungu atuumbie roho iliyopondeka kama ile tuliyokuwa nayo mwanzo na kuzidi, katika jina la Yesu.

Comments