Skip to main content
MUNGU ALIMLETA HUYU KIJANA ILI NIMWOMBEE NA APONE
 

 
Ngoja leo ni mshuhudie kuhusu miujiza ya BWANA   YESU:
 Siku 1 nimeenda kufanya maombi mlimani
 Nipo peke yang kileleni mwa mlima,nikawa nasujudu,mara nikasikia sauti kama mtu 
anatembea,nikajipa moyo nikisema kama ni mnyama,nyoka,mtu MUNGU 
ataniokoa,sauti ikanyamaza nikamaliza kuomba niangalie kwa uwoga unajua 
kibinadamu,alafu jioni sana,namwona kijana amesimama ananishangaa 
kweli,nikamkaribisha tuombe,akakubali,hizo shida zake 
alizonielezea,machozi yalinitoka ni MUNGU alinikutanisha naye,namhoji 
kama amekuja kusali,ananiambia,anapoteza mawazo,amekata tamaa ya 
maisha,embu tafakari si alikuwa amekuja kujiua yule aisee,nilimtizama 
nikahema,nikampa moyo nikamwambia kama huyu MUNGU  aishivyo leo ni siku 
yako,aliniambia kila alichofanya afanikiwi,analaumiwa kwao,hana 
kazi,anaongea machozi yanamtoka
 Hadi mimi machozi yalinilengalenga,nikapiga 
naye magoti,nikaomba toba,Roho ananiongoza katika sala,kumbe ni mizimu ya 
ukoo(babu) yani ujue watu wamekamatwa hawajijui,niliposema  tu wewe 
mzimu,elewa tumepiga goti,na kufunga macho,nilisikia kivumbi kama kuku 
anayechinjwa,anagaragara chini,naomba huku nimefumba macho nilisikia kishindo 
kama mabawa lindege likubwa likiruka hadi nikasisimuka,namalizia 
amen,jamaa namkuta amezirai,namgusa aamke,hajitambui ananisalimia kwa 
uwoga,kumbe hata alikuwa fahamu zake hazipo kama yupo mlimani,nikapiga 
kimya,nikamwambia karibu,nipo ndo naomba ila nenda kamshukuru Mungu upo 
huru sasa,yani niliteremka mlimani nasema ni nini hii,hapo nimeenda 
kujiombea na mambo yangu.
 Nawe leo jitoe kwa wengine,umejua Mungu anakutumia usirudi nyuma,kazana uwe msaada kwa wengine katika jina la Yesu. Amen!.By David Polle


 
 
 
 
 
 
  
 
 
 
 
 
Comments