Shuhuda ya kijana Eliya ambaye alikuwa akiishi na jini bila kujua..
Eliya :-
Nilikuwa
zanzibar kibiashara na nilikuwa nafanya biashara ya kuuza computer,
ambazo nilikuwa nazifuata huko. Nikiwa katika mapumziko Zanzibar maeneo
ya forodhani, na wa dada wawili wakaja wakaniambia tunahitaji kampani,
kwakuwa nilikuwa bar. Wakiniuliza una mtu, basi nikasema hapana, basi
wakaja na tukaanza kunywa, baada ya muda tukiendelea kunywa. Wakaniuliza
jina langu na shughuli zangu, nami nikawatajia.
Kesho
yake asubuhi wakati nimetoka kutafuta riziki nyuma yangu, nikashangaa
imesimama gari, na nikawaona wadada wale wale ambao niliwaona jana yake.
Basi waliniomba niende nao nikawambia naenda kazini, wakanisihi ninywe
nao supu. Basi baada ya hapo siku ile ikapita tena.
Siku
moja nikiwa mwenge, gari aina ya vx lilipaki karibu nami ( namna
alitaja ila tunaziifadhi) . Na pale akatoka yule yule binti aliyemuona
Zanzibar na safari hii alikuwa mmoja. Nikamwambia naenda ofisini.
Akaniambia tuingie kwenye gari na nikapanda. Na Yule binti akanipeleka
hotelini, basi yule binti akaniambia Nina kitu cha kunieleza
nikamshawishi aniambie. Basi akaniambia kuwa anaomba tuwe marafiki ,
basi nikamkubalia na nikaanza kumchukulia kama dada yangu. Basi
tukaondoka na kuendelea kuwasiliana. basi baada ya siku chache nilienda
zanzibar na Yule dada alinisaidia kutafuta mzigo na badala ya kukaa siku
tano akakaa siku tatu........
.......ameruka baadhi ya matukio kwaajili ya muda kuwa mdogo.....
Nilikuwa
msaada kwake kwa kipindi cha mwanzo, lakini baada ya muda, Mimi ndio
nikaonekana ndiye ninaye hitaji msaada, kwa kuwa alikuwa na hela ambazo
awali hakujidhihirisha.. Mwanzoni alikuwa Kama mtu asiye na hela.. Akawa
ananipa hela siku baada ya siku. Basi nikafanikiwa kujenga nyumba mbili
mlandizi, na baada ya hapo nilishangaa alikuwa anaendelea kunipa pesa,
mwanzoni alinipa laki 7 lakini ilifikia kipindi ananipa hadi sh.
Milioni 40.. Na bila kujua anatoa wapi kwakuwa hakuniambia anafanya kazi
gani. Na hapo huyo msichana akanipa gari, alinipa vitu vingi. Na baada
ya muda mazoea yakazidi basi nikamshirikisha kuwa kama inawezekana tuwe
pamoja kama mtu na mchumba wake. Alikubali na kwa wakati huo nilikuwa
sijui anapoishi na hapo nikamuuliza akaniambia baba na mama yake wako
Nugwi Zanzibar. Basi tukakubaliana tuanze kwa kwenda kwa wazazi wangu
ambao wapo singida,
Tukapanaga safari , tukiwa
safarini kuelekea singida, Dodoma. Akapotea ndani ya gari tulilokuwa
tumepanda. Maana yeye alikuwa amekaa siti ya dirishani hapo ,
nikawauliza abilia wengine nao walikuwa hawajui, . Na mara wakati
tunajadili yule binti aliyekuwa akiitwa Hawa, akarudi . basi kukawa
kimnya kila mtu alikuwa anaogopa. tuliposhuka kwa mapunziko mzee mmoja
ambaye alikuwa abiria akaniambia nishuke.. Maana nitawaletea matatizo.
Nikashuka naye baada ya kunisisitiza abiria kunisisitiza.
Tukiwa
dodoma, nikatamani nimuone mguu wake, maana niliambiwa awali kuwa jini
anakuwa na kwato. Kwa kuwa kwa wakati huo nilikuwa sijawahi kuona miguu
yake, tokachukua chumba pale Kilimanjaro hotel Dodoma, akatoka kidogo,
lakini nilimvizia akirudi nione miguu yake, cha ajabubbaada ya kurudi
Yule binti akakataa kupumzika na alikataa kuvua viatu pia. Basi kwakuwa
alikuwa na nguvu kunizidi basi nikapanga kumkimbia, kwa kuwa nilianza
kuingiwa na hofu, nikamwambia kwa kumdanganya kuwa naenda kununua vocha.
Lakini nilipotaka kukimbia kufika getini nikakutana naye anatokea
ninakoelekea. Basi ikabidi nirudi ili nimuangalie miguu asubuhi wakati
wa kuamka, Asubuhi nilipoamka yeye akaniwekea mkono kichwani hapo
nikalala hadi akaoga akamaliza. Nakuja kuamka baada ya masaa bila kujua
usingizi niliupatia wapi..
Basi kesho yake
tukapanda gari lingine la kuelekea singida. Tukiwa njiani, manyoni
polini, ghafla akaanza kupiga kelele akisema sitaki kwenda kwenu siwezi
kwenda, na sitaki kwenda.. Basi gari likasimama manyoni singida na kwa
kuwa sikuwa na jinsi ikabidi nishuke na tulipofika tu akatoweka tena.
hapo nikasema sina jinsi zaidi ya kukimbia nikakimbia umbali kama wa
kutoka Kawe hadi ubungo kufika tu nataka nipumzike nikamuona kutokea
mbele, na akawa ananihoji unaenda wapi.. Nikamuomba msamaha nikataka
kwenda polisi nikakutana naye anatoka polisi. Nikawa sina jinsi zaidi ya
kumtii tu. basi tukarudi dodoma, na hapo akainua mikono yake ikamwagika
kitu Kama maji, akanimwagia mguu akiniambia tutaona nani baba Kati yako
na Mimi. Baada ya hapo .. Yeye aka toweka
Nikiwa
Dodoma nikaamua kutafuta kanisa.. Kwakuwa alikuwa amechukua hela zote,
Na nikapata kanisa nikamwelezea Mch. Na akaniombea na akaniambia
nipumzike na ghafla yule binti akatokea hofisini nilipomuelezea Mch. ,
mchungaji akakimbia kutoka ofisi na Mimi nikakimbia kumfuata mchungaji
basi Yule Mch. Akaniambia kamtafute pastor Max. Wa ufufuo na uzima ndiye
atanisaidia kwa kudai Mimi nitamletea matatizo.
Basi
walinipa nauli kidogo na nikaja dar. nilipofika dar. Nikaenda kwenye
nyumba yangu mikocheni nikaenda lakini sikuikuta tena eneo amabalo
ilikuwepo awali. Na nikaamua kuja kumtafuta Mch. Max. Basi nikaja
kanisani na nikaombewa japo nilikuwa sina imani kabisa ndani.

Comments