NILITAKA KUFA BAADA YA KUIKATAA PESA MBOVU YA BIBI MMOJA NIKIWA NAUZA DUKA

PETER MICHAEL

BWANA YESU asifiwe wapendwa, mimi ni mzima na namshukuru MUNGU kwa neema yake .ndugu zangu naomba niwambie jambo la kweli ambalo lilinitokea. Baada ya kumaliza kidato cha nne mwaka 2005 kule Biharamulo sec school mwaka 2005 nilienda nyumbani Misungwi Mwanza na pale nyumbani kulikua na duka ambalo halikua na muuzaji kwa muda huo hivyo nikapewa jukumu hilo la kuuza duka. na nilianza dec 2005 hadi nilipoenda JKT feb 2007. Sasa kipindi nauza duka nakumbuka ilikua June 2006 nikiwa nauza duka kama kawaida alikuja bibi mmoja muda wa saa kumi jioni  ambaye namfahamu anaishi nyumba ya nne kutoka dukani bibi yule alikua na Tsh.100 na alitaka mafuta ya taa nikampimia mafuta na akanipa pesa nikakuta ni pesa nyusi sana na imeharibika sana hata hakuna mtu anaweza kuikubali nikamwambia yule bibi anibadirishie ile pesa na anipe nyingine akakataa na kusema hana pesa nyingine, nikasemwambia tena basi namkopesha mafuta ataniletea pesa akakataa tena na kusema hataki kukopa, nikamwambia tena basi nampa mafuta hayo ya shiling 100 bure akakataa na kusema hataki vya bure nikamuuliza kwamba anataka tufanyeje akasema nichukue hiyo pesa. Moyoni mwangu amani ilianza kupotea na rohoni ni kama nilikatazwa kuichukua hiyo pesa akanilazimisha nichukue hiyo pesa nikakataa na kumwambia achukue mafuta na hiyo pesa yake bure yule mzee akawa na hasira sana na kuniambia kwa kisukuma kwamba ''WAILEMA E HELA IYII BASI UKUISANGA LELO KWIGURU'' yaani ''UMEIKATAA PESA HII BASI LEO UTAIKUTA MBINGUNI'' yule bibi mwenye kama miaka 70 au 80 baada ya kusema hivyo akaondoka haraka haraka sikumjibu kitu ila nikapuuzia maneno yake.Niliendelea duka kuanzia hiyo saa kumi hadi saa mbili usiku na hakukuwa na tatizo lolote. Ilipofika kama saa mbili na dakika 10 mara baada ya taarifa ya habari kuisha maana nilikua nasikiliza radio nilisimama na kumhudumia dada mmoja na mtoto mmoja waliokuwa wanataka vitu vya dukani na ndani ya duka kulikua na taa upande wa juu na mara kwa mara usiku huja wadudu karibu na taa na hilo ni jambo la kawaida tu sasa nikiwa napanga nikimaliza kuwauzia hawa wateja wawili nifunge duka ghafla alitoka mdudu kwenye taa na kunidondokea mgongoni na niwadudu wa kawaida na wa siku zote lakini siku hiyo ilikua ya tofauti kwani aliponiguza tu yule mdudu mdogo mgongoni kwangu niliishiwa nguvu na kushindwa hata kugeuza macha au kusogeza mguu au hata kugeuka maana nguvu zote ziliisha ila tu mdomo uliweza kuongea. niliduwaa nikiwa nimesimama huku sina nguvu hata chembe nikadondokea kwenye kiti ambacho hua nakalia nikiwa nauza dukani ajabu ni kwamba wale wateja wote hawakujua kinachoendelea na waliendelea na  kuniambia ''tuludishie basi chenji tuondoke au unataka kutudhulumu?'' niliwaambia waniitie kijana mmoja wa nyumbani anayeitwa Sumbu anisaidie kufunga duka na kweli kama dakika 3 Sumbu akaja nikamwambia aingie dukani na wakati huo nikapata nguvu kidogo nikatoka nje na kuanza kufanya mazoezi kana kwamba ndio kwa mara ya kwanza naanza kutembea nikiwa nje wateja walikuja isivyo kawaida kwani walikuja wateja zaidi ya 15 tena huku wengine wakiendelea kuongozeka hii haikuwa kawaida nilihisi ilikuwa mbingu ya shetani kuleta watu ili nfe kabla ya kwenda nyumbani nilipata nguvu kidogo na kumwambia sumbu kwa ukali kwamba afunge duka bila kuuza chochote ,wale wateja walinishangaa sana na kuanza kusema nimeanza kulinga ila hawakujua nini kinaendelea. baada ya kufunga duka simbu alinishika mkono na kuanza kunisaidia kutembea tulitembea huku sumbu akinishangaa na kuniuliza kuna nini kimetokea? nikasema nitamwambia baadae. Tulipofika nyumbani nilimweleza mama naye akahamaki na kuchukua panga na kumwita kaka yangu Samwel kwamba wamfuate yule bibi  walipotoka tu nje ya geti wakakutana na jirani yetu mzee nyanda akiwa na mke wake wakamweleza na kuanza kujadiri jinsi ya kufanya lakini maamuzi waliyofikia ni kurudi kwanza na kuniombea maana hali yangu ni mbaya sana hata kuongea ni tatizo. Waliniombea na wakati wanaomba nilihisi kuna kitu kinachomoka mwilini mwangu na nikawa wa tofauti tena nikawa mzima hata nikashangaa kwamba MUNGU anasikia maombi na kujibu sekunde hiyohiyo nikawa mzima kabisa ila tu hofu ikaendelea kutawala moyoni mwangu na usiku huo sikulala maana nilidhani nikifumba tu macho kulala wangenichukua wacahawi wale.Kesho yake baba alikuja maana jana yake hakuwepo alikua mwanza mjini kikazi na alipofika alimwita yule bibi pamoja na mimi na kuanza kumsikiliza kila mmoja na yule bibi alikana na kusema hakuja dukani kwangu labda nimekua kichaa nilisema yote alichofanya tu yule bibi ni kuomba msamaha huku akisema hajaja dukan. Baba alisema basi yule bibi asije tena dukani na yule bibi alikubali maana alimwogopa baba kwa sababu baba alikua mmoja wa wakubwa katika halmashauri ya wilaya na alikuwa anaheshimika sana. Baada ya wiki moja yule bibi alikuja tena dukana na hofu kuu ikanijaa maana alikuja kukiwa hakuna mteja yeyote zaidi ya mimi muuzaji na akaniambia kwamba nina bahati maana YESU wa mama na ndugu zangu amenisaidia zaidi ya hapo andeniua na akasema nimshike sana huyo YESU lasivyo lazima aniue maana nimemtangaza sana kwa watu baada ya tukio lile la pesa mbovu, sikusema neno lolote hadi akaondoka baada ya hapo niliamua sasa kumwamini BWANA YESU maana nilijua nikicheza nakufa  na baada ya miezi 4 nikaondoka misungwi na kwenda JKT na kama unavyojua vijana wengi kwa sababu ya kupenda ya dunia nilirudi nyuma baada ya tatizo kuisha lakini namshukuru MUNGU kuokoka nov 2008 hadi sasa nasonga mbele na katika maisha yangu hakuna kama BWANA wetu YESU KRISTO kwani kaniokoa na kuniondoa katika utawala wa shetani na sasa mimi ni mtoto wa MUNGU kupitia yeye ni mimi ndugu yako Peter Michael . MUNGU awabariki sana  na kama hujaokoka basi wakati wa wokovu ni sasa hivyo chukua hatua.

Comments