![]()  | 
| MOJA YA MAMBO YANAYOUMIZA WATU WENGI NA KUACHA MAJERAHA MENGI NI VITA MFANO HAWA NI M23 HUKO WAKIWA GOMA MASHARIKI YA KONGO MAZINGIRA KAMA HAYA YA VITA HUACHA MAJERAHA MENGI SANA | 
Moyo wangu hauna nguvu wala nafasi ya kubeba chuki dhidi ya walionikosea katika maisha yangu yaliyopita.
 Mpendwa je wewe ni mtu ambaye kuna watu wame/likukosea kila ukikumbuka walivyokufanyia unashindwa kuwasamehe?
Kama wewe ni miongoni mwa wasioweza kusamehe ningependa kukufahamisha kuwa unapohifadhi chuki moyoni mwako anayeumia ni wewe.
Mbali ya kuwa kuhifadhi chuki kwa kushindwa
 kusamehe kunaweza kukuletea  maradhi kama vidonda vya 
tumbo,depression,magonjwa ya moyo n.k pia  ni chukizo mbele za Mungu.
Kabla hujaendelea kuwawekea vinyongo watu 
waliokukosea inabidi ujiulize je ni mara ngapi umemkosea Mungu lakini 
kila ulipotubu alikusamehe na kusahau kabisa?
Wakati mwingine mtu anaweza kuwa yeye ndiye
 aliyekukosea ila akawa anajitahidi kuwashawishi watu tena kwa machozi 
juu  LOL kuwa wewe ndiye uliyemkosea ili watu wakuone kuwa wewe ndiye 
mbaya.Hata watu wa aina hii pia ni wakuwasamehe na kukabidhi kila kitu 
kwa Mungu.



Comments