UNA NINI MKONONI?

GASPER MADUMLA



Kutoka 4 :2
“ Bwana akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, Ni fimbo. ”
Musa alikuwa na kitu cha tofauti kabisa na chenye thamani ambacho kinaweza kumuokoa yeye mwenyewe na taifa lake lote na si kingine bali ni FIMBO ambayo yeye alikuwa nayo lakini alikuwa hajui kama FIMBO hiyo ni ya thamani kiasi hiko,

Hii inamaana kuwa hata wewe yamkini unafimbo mkononi mwako lakini ambayo wewe kwa akili zako haujafahamu umuhimu wa fimo hiyo,sasa ili uweze kufahamu ni lazima ufunuliwe na Roho mtakatifu.

Kila mmoja aliyekuwa na Kristo Yesu ndani yake ,ana fimbo mkononi mwake ila tatizo ni kwamba hujajua kwamba fimbo hiyo inaweza ukaitumia kujikomboa wewe na taifa lako kwa msaada wa Mungu kama jinsi ilivyokuwa kwa Musa.

Sasa tazama mstari huo pale Mungu anapomwambia Musa kwamba aitupe chini kisha anamwambia “ BWANA AKAMWAMBIA MUSA,NYOSHA MKONO WAKO,KASHIKE MKIA ” Kutoka 4: 4

Sote twafahamu kwamba,endapo utamshika mkia nyoka, yeye atakunga’ta, lakini tunaona Bwana Mungu anamwambia Musa akamshike mkia ,
Hapa kuna fundisho kubwa sana tena sana..
Ooooh HALLELUYAAAA…

Tunajifunza hapa kwamba MUNGU HAWEZI KUKUPA KAZI AMBAYO ITAKUSHINDA MAANA KILA KAZI AKUPAYO YEYE AMEKWISHA KUIFANYA KWANZA NA KUIMALIZA,

NDIPO ANAKUPA WEWE,TENA HAKUNA BAYA LITAKALOKUZURU WEWE IWAPO BWANA MUNGU ATAKUWA UPANDE WAKO,
hata kama ni nyoka,huyo umwonaye kwa macho yako ni nyoka kweli,lakini mbele za Mungu si nyoka bali ni kumbi kumbi tu,Ndio ninakuambia ni kumbi kumbi tu

Yaaaaaaaa! Come ooon !
Shout Haleluyaaaaa…
Ninakuambia katika mwaka huu,yale uyaonayo mfano wa nyoka kwa macho yako ya nyama katika ulimwengu wa roho si nyoka bali ni panzi ikiwa Bwana Mungu akiwa upanda wako na hakuna cha kukutisha

Tunasoma Zab 118 :6
“Bwana yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? ”

Pia ZAB 46 : 1-2
“ Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. ”

Mungu hawezi kufanya jambo lolote kwako nje ya kanuni ya IMANI
• Imani ni mkono wa kupokelea mbaraka wako
• Imani ni mkono wako wa kukuvusha hapo ulipo,Imani ni FIMBO

Sikia;
Nje ya Imani hakuna jambo lolote,
thus why,Biblia inatuambia kwamba kila kitu kitafanyika kwako kwa kadri ya imani yako.

Ok,

Fimbo uliyonayo wewe ni kwa ajili ya utukufu kwa Bwana na si kwea ajili ya kujipatia sifa wewe wenyewe ,Tazama jinsi Mungu anavyomwambia Musa kwamba fimbo hiyo ni kwamba Mungu wa Ibrahimu ,Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo amekutokea.

Ili muujiza wako,au ili wokovu wako ukomae ni sharti utumie fimbo yako vizuri la sivyo hakuna MPENYO wowote,Na hii ni kanuni ketu sisi wanafunzi wa Yesu, Kwamba hiki tulichonacho kidogo chatosha kuzidishwa,maana Mungu wetu ni Mungu wa kuzidisha na wala si Mungu wa kuongeza.
Tofauti ya KUONGEZA na kuzidisha ni hii ;
• Kuongeza,6 +6 =12 But,
• Kuzidisha,6*6=36
Umeona hapo,
Halleluyaaaaaa……

Tazama mfano mwingine wa kuzidishiwa kwa kutumia fimbo uliyonayo;

Tunasoma Marko 8 :5
“ Akawauliza, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, ”

Hata wewe unakitu cha ziada hata kama haujakijua,ila ukimshirikisha Roho mtakatifu Yeye atakuambia cha kufanya
Tazama hata hili limejitokeza kwa KOLNERIO alikuwa ni mchaji wa Mungu, na alikuwa ni mtoaji mzuri ,lakini ilikuwa hiyo haitoshi peke yake.

Maana alikuwa na kitu au fimbo ambayo aliitambua tu pale Roho mtakatifu alipowashukia yeye na ndugu zake pindi Petro alipotumwa na Bwana Mungu ( Soma Matendo sura yote ya 10 )

• Wakristo wengi wanakufa na njaa hali wana kitu cha ziadamikononi mwao ,yaani wana fimbo ya kuweza kuwatoa mahali walipo,
• Wakristo wengi wana TARANTA lakini hawajitambui thamani ya taranta zao,au hawajui kabisa kama wana tarantahizo.

Hii haiwezekani mpaka umsihi sana Roho mtakatifu akufunulie hiyo FIMBO yako uliyonayo,nawe uitumie kwa kadri yaYeye atakavyo.

Oooooh,Bwana Yesu asifiwe….
Nimefurahi sana maana naona Bwana Mungu anazungumza na wewe,kuhusu kile ulichokuwa nacho,hiyo ni fimbo yako nayo yaweza kuwa nyoka pia yaweza kurudi katika hali yake nakukuokoa wewe pamoja na famili,majirani na ukoo,pia na taifa lako loteeee,

Ayayayayaaaaa,Halleluuuuyaaaa.
. some body say AMEEEEEN,
Pokea katika Jina la Yesu Kristo,
Chochote unachotaka kuanzisha wewe anzisha katika Jina laYesu,huku Yeye ukimweka mbele nawe utafanikiwa.

UBARIKIWE..

Comments