![]() |
NGUVU YA MUNGU AU UPAKO WA KIMUNGU UKIWA UMESHUKA NA KUPONYA WATU AMBAO MIKA MINGI WALIKUA VILEMA NA WAGOJWA LAKINI NGUVU YA MUNGU ILIPOSHUKA WAKAPOKEA UZIMA KATIKA JINA LA YESU |
UPAKO WA MUNGU: upako wa kimungu ni nguvu ya Roho mtakatifu inayomwezesha mtu aliyeokoka kufanya mambo makubwa yasiyo ya kawaida yaliyo nje ya uwezo wa kibinadamu,na kama tunasema kuna upako wa MUNGU basi tambua hata upako wa shetani upo pia na wapo pia ambao ni mawakala wa shetani ambao nao hufanya miujiza ya kipepo lakini kwa wanaoongozwa na ROHO MTAKATIFU lazima tu watabaini kwamba huyo ni shetani na sio MUNGU lakini kwa leo sizungumzii upako wa shetani bali upako wa MUNGU ; waamuzi 14:5-6 ......... Roho ya BWANA ikamjilia kwa nguvu naye akampasua kana kwamba mwana mbuzi..........; biblia inasema upako wa MUNGU ulipomshukia samson akawa na nguvu na kumwua simba kana kwamba ni mbuzi hiyo inamaana upako uliposhuka samson alimwua simba kirahisi sana hivyo tumwombe MUNGU BABA atupe upako huu ili tuweze kushinda adui zetu wote kama magonjwa,umaskini ,mabalaa na kila hila za shetani. pia kumbuka jinsi Daudi alivyomshinda goliath baada ya Roho ya MUNGU kuwa juu yake 1samwel 17:49-50, kwa akili yake asingeweza kumshinda goliath. pia kumbuka biblia katika zaburi 69:12 "kwa msaada wa MUNGU tutatenda makuu maana yeye atawaseta mbali watesi wetu" balikiwa sana mtu wa JEHOVAH kwa ujumbe huu
Comments