
Basi baada ya muda baba akawa
anasema mtaani, kuwa eti najidai na hela. Na kuwa mama yangu ananipa
kiburi. Na Huo ulikuwa mwaka 2004 na baada ya muda nilipigiwa simu kuwa
baba mkwe anaumwa. Kwa hiyo mke wangu akaamua kwenda lakini alipofika
akaanza kuwashwa sana na akaanza kuumwa. Basi nikamwambia mke wangu
arudi nyumbani, kwa kipindi kile nilikuwa mwislamu safi. Basi kumbe kule
nje baba yangu akawa akasema mke wangu ndio ananiletea kiburi ili
nisimsaidie. Na atanionyesha Mimi na huyo mke wangu.
Kwa
kuogopa nikaamua kuhamia dar es salaam, basi mke wangu akazidi kuumwa
nikampeleka hospitali nyingi , Kama muhimbili, Kenya, bugando na kcmc na
hapo nikamwacha hospitali ya kcmc bila kuwa na matumaini kwa kuwa
madaktari walikuwa hawajui ni aina gani ya ugonjwa unaomsumbua. Basi
nikarudi dar. Kuangalia watoto.. Maana ilikuwa miezi minne nazunguka
hospitalini. Basi kulikuwa na daktari mmoja mkongo akasema mke wako ni
msukule mpelekeni kwenye maombi, na kwasababu kwa kipindi hicho nilikuwa
mwislamu swala tano, sikukubali aende hospitali.. Basi baba aliendelea
na maneno kuwa mke wangu lazima afe hata nimpeleke wapi. Akasema kuwa
hata nimpeleke nje ya nchi atakufa tu.
Baada ya
siku mbili baadaye mke wangu akafa, basi baba yangu akaja msibani , cha
ajabu nilipomaliza kuzika tu, baba sikumwona tena. . Basi baada ya
kumzika mke wangu , siku nne tu wakaja mashehe wengi sana nyumbani
karibu kumi na kitu hivi. wakanishawishi nioe tena, nikawambia yaani
siku nne tu mnanishauri nioe tena. Nikakataa kuwa sitaoa tena.
Ghafla
siku moja nikiwa nimelala nyumbani nikasikia mlango ukigongwa, na
mlangoni nikasikia sauti ya mke wangu ikinisalimia, nikakimbia kufungua
mlango na cha kushangaza sikumuona mtu, hapohapo nikaanguka na kuzimia
,sikuamka mpaka kesho yake.. Na nilipoamka nikakuta mashehe wengi
nyumbani, wakaniambia huo ni mzimu wa mkeo, wakaja na madawa mengi
wakaniambia nitumie ili nimsahau nikakataa kutumia madawa yao nikasema
mke wangu hajafa.
Basi kwa sababu ya uoga
nikawaita ndugu zangu karibu 6 , nyumbani kwangu. siku moja nikiwa na
ndugu zangu tumelala sebuleni, usiku mke wangu akanitokea tena.. Na hapo
alipotokea nikamfinya mdogo wangu ili aamke naye aone lakini hakuamka
wala kusikia, mke wangu akaniambia saa ya ukombozi imefika. Na hapo
tuliongea karibu dakika 45. Baadaye nikamwambia natakaka nije alipo
nilipomfuata akapotea na sikumwona. Nikaangusha friji na meza. Ndipo
ndugu zangunwalipoamka. Na asubuhi mkono wa mdogo wangu ulivimba kwa
vile nilvyokuwa nikimfinya..
Basi nilikuwa
mwislamu mzuri kipindi hicho , nikamwambia mama kiongozi wa kiislamu,
naye akaniambia niombe dua ili asipatikane tena. Akaniambia nitumie
ubani, ili kumfanya asinitokee tena. Mimi nikamkatalia kwa kumwambia
siwezi omba hiyo dua maana mke wangu hajafa.
Siku
moja nikiwa nimepanda kwenye gari, nikazozana sana na konda, na hapo
nilikuwa narudi dar . nilikuwa nimepanga nikifika dar. Niende nimpige
risasi baba, basi ndani ya gari nilikuwa nimekaa na mzee fulani simjui ,
akanisii sana nimuelezee matatizo yangu, nikakataa lakini nikajikuta
nimemueleza. Na nilipomwambia ,akanielekeza niende kanisani ufufuo na
uzima. na nikakutana na Mch Adriano .bakaniombea na nikawa naendelea
kuja na mkesha. Ingawa sikuwa na imani kubwaa..
Ijumaa
moja nikiwa kwenye mkesha akaletwa mama mmoja aliyekuwa amekufa,
tukaenda kumuombea nikapenya kuona kama amekufa kweli, nikamgusa alikuwa
amekufa basi baada ya maombi kama saa hii akafufuka, lile jambo
likanipa imani kubwa sana.. Na ndipo imani ikaiingia kuwa mke wangu
anaweza kurudi.
Sikuchache, baadaye nikapigiwa
simu kuwa mke wangu ameonekana anaosha vyombo boko. Na hapo nilienda
nikakuta mwenye kibanda kile amefunga kibanda na hayupo tena amekwenda
same. Na huyu mama alikuwa rafiki wa familia yetu kwa kuwa alikuwa
karibu na baba yangu. Kifamilia nikashangaa kumbe ndiye aliyekuwa
amepanga mbinu moja na baba.... Na hili ni tukio lililotokea kama wiki
tu imepita.... Naamini Mungu anaweza... Na atamtudisha mke wangu....
Comments