Skip to main content
USHUHUDA,AMINI KATIKA JINA LA YESU
Baada ya kumaliza chuo cha utalii,nilitafuta kazi kwa shida sana,Arusha. Niliwajua wengi lakini hawakuweza kunisaidia.
Ipo siku sitosahau nikawa najiombea sana hadi usiku mnene,sikujijua au
Mungu anakusudi gani nami. Nina shemeji yangu alikuwa meneja mwajiri
katika kampuni ya Utalii,nilimwomba sana anisaidie,lakini kazi
zilikuwepo,hakunisaidia. siku moja akanipigia simu,nikamfuata, akaniambia kuna
kazi imepatikana,Bukoba utaweza kwenda,nikamjibu ndiyo,sikuwa na jinsi
miaka 5 nipo mtaani,nasota. Akaniunganisha na huyo mwajiri,akanitumia
nauli,nikaenda Bukoba. Nikapokelewa vizuri,nikapewa nyumba ina kila
kitu. Nikapewa na cheo nikawa meneja. Sasa nilikuwa sijajitambua,wakati
mwingine naona maono ya Mungu,napuuza,nikaanza kazi nilikuwa napata
wageni wazungu,nafanya kazi,pesa ikanikolea,sikuacha kuomba,nikasahau
nilipotoka nikaanza kunywa pombe,wasichana,lakini kila nikinywa,usiku
nateswa kwenye ndoto naona majitu yananifuata,nanyongwa,wakati mwingine
wananibeba kama kunipeleka sehemu inagiza,nalia kweli na uwanaume
wangu,nashituka nabadilisha mwenendo,naacha pombe,nikiacha uovu nalala
vizuri kumbe hayo yote ni Mungu alinipenda,wapo wengine wanakufa.
Nikatubu nikarudi kundini,nikawa makini,jinsi nilivyokuwa nalewa bosi
alinifurahia sana,alinipa hadi usafiri,niliposimama kimaombi,kila nikienda
kazini ananilalamikia,mara anasema sifanyikazi nastarehe,nikawa
nasonöneka,nikapata marafiki wa kanisa fulani,wana wazungu wakawa
wananipa kazi,tajiri yangu alikuwa ana Hotel,siku moja
wakanialika,mchungaji nikale pasaka,katika maongezi Bwana mmoja
akaniuliza,hapo kwenu hamna kazi,nikamjibu hamna,akaniuliza kuna msanii
alikuwa anaimba alikufa pale,wanavyodai alitolewa kafara. Wakaniambia
uwe makini bana,dah! Nikashtuka na yale mauzauza niliyokuwa nayaona
usiku. Nikatulia nikaanza kukesha,maombi. Bosi mkubwa
hakuwepo,nikapigiwa simu anakuja,nikaenda kumpokea. Nikawa naye siku
3,ikawa jumapili siingii kazini,akanipigia simu,wewe umekuja kustarehe,au
kufanya kazi,nikaenda kazini sikumjibu,navyokwambia nilikutana na barua
jumatatu ofisini,ya kwamba nimeachishwa kazi. Nikapokea mshahara wangu
nikarudi Arusha. Ndipo nilipoamini maneno ya wale wachungaji,kusimama na
Mungu ikawa vita pale hadi nikafukuzwa kazi. Ushuhuda huu uwajenge,muwe
mnamuuliza Mungu au kumshirikisha awape kazi,usikurupuke wengi
wameajiriwa na makampuni,wamekuwa watumwa,hakuna wanachokifanya,baada ya
hapo nilianza kujiajiri mambo hayaendi,kumbe Mungu ananiita,ipo siku
nikachoka na tabu hizo,nikamwomba Mungu japo anionyeshe kazi
nitakayokuifanya,kweli Mungu ni mwaminifu,niliota ndoto nawaombea watu
vibaya mno,nilipoamka nililia sana,nikwamwambia Mungu umeniacha siku
zote nateseka,kumbe ulinihitaji. Huenda ni wewe ndugu,usione unapita
kwenye mapito sana,tuliza moyo wako,mwambie Mungu atakupa kazi
yako,tunajipotezea muda kwa kuangalia matatizo yetu. Ukiwa na
Mungu,aliyekuajiri ni mchawi au mshirikina,ataambiwa na bwana wake,nao
watakutesa,pasipo wewe kujijua,utapata mshahara leo,pesa itaisha
kesho,chuma ulete,tuombe sana Mungu.
Bwana Yesu atusaidie ahsanteni. Kwaherini Aminaa!.By David polle
Comments