YESU KRISTO PEKEE NDIO MWENYE MAJIBU YA MATATIZO YAKO







Hakuna mwanadamu yeyote mwenye majibu ya maisha yako, hata hao unaodhani wana majibu yako, unapowaelezea matatizo yako, wanajiuliza maswali mengi kuhusu wewe na hawapati majibu, wanaishia kukupa majibu yasiyo sahihi. MUNGU pekee ndiye ana majibu ya maisha yako kupitia YESU KRISTO, (Mathayo 11, watu waliona Lazaro ameshakufa na majibu waliyokuwa nayo ni kwenda kumzika, lakini Yesu alitoa majibu sahihi, kwamba Lazaro ataishi tena hata kama alionekana ameshakufa). Yesu anajua ni kwanini uko hivyo ulivyo, anajua sababu ya wewe kuwa hivyo, japo watu wamekupa majina ya ajabu ajabu, usiogope! Neema ya Mungu iko kwa ajili yako ndio inayoweza kubadilisha historia ya maisha yako mpaka watu wabaki midomo wazi...! (1Wafalme 19:4-8, Japo Eliya alikua ameshakata tamaa kabisa, lakini Neema ya Mungu ilimfuata pale chini ya mretemu na kumfanya akaishi tena). Mwambie Mungu....."Nahitaji Neema yako, maana ndiyo inayoweza kubadilisha historia ya maisha yangu.. Naomba uninyeshee mvua ya Neema yako JEHOVA, kwa jina la YESU KRISTO Amen". MUNGU akubariki sana

Comments