ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA |
Huu ni mwendelezo wa somo la KERUBI AFUNIKAYE, EZEKIELI
28:13-18.. Kerubi ni aina malaika
wanaobeba uwepo wa BWANA, Ni malaika wa ngazi ya juu.. mbele za BWANA. Maana malaika wapo katika ngazi tofauti ndiyo
maana katika kitabua cha ISAYA wametajwa malaika aina ya MASERAFI, na pia YUDA
1: Kitabu hiki kimetaja Mikaeli kama
malaika mkuu kumbe kama kuna malaika mkuu basi chini yake kuna malaika wengine.
KWELI KUHUSU MALAIKA:
Kuna malaika wa ngazi tofauti, kama tulivyosoma kwenye YUDA
1:9 na DANIELI 12:7 Ttunaona wamemtaja
malaika Mikaeli kama malaika mkuu, na katika ISAYA 6:1—BIBLIA inasema kuna
malaika wanaitwa maserafi ambao wao ni malaika wanaokaa karibu na BWANA ambao
Isaya aliwaona kwenye maono, na pia kuna Makerubi AMBAPO shetani alikuwa katika
ngazi hii ya malaika. UFUNUO 12:7
Mikaeli kama malaika mkuuwa vita, chini yake ana malaika wa ngazi mbalimbali.
Na ndio maana katika kitabu hiki cha UFUNUO 12 tunaona jeshi la malaika
waliochini ya mikaeli.
UNAPOOKOKA MALAIKA
WANAKUWA UPANDE WAKO:

Malaika wanatenda kazi kwaajili yetu na ni watumishi wetu.
Kuna malaika mwingine mkuu wa taarifa anaitwa Gabrieli huyu ni malaika mkuu wa
taarifa naye ameonekana kwenye biblia sehemu nyingi akileta taarifa mbalimbali,
yaani unaweza ukapitia kwenye kipindi kigumu ukiwa hujui la kufanya basi huyu
hutumika kuleta taarifa za kimungu kwetu. HATA Danieli alipofunga siku 21 akiwa
haoni matokeo yoyote Malaika aliyekuja kuleta taarifa kwa Danieli. Mikaeli ni
malaika anayetupa taarifa za kutoka mbinguni. Ndio maana hata kama watu
wanakupiga vita kwa siri usiogope maana tuna malaika Mikaeli
KERUBI MWENYE KUTIWA
MAFUTA AFUNIKAYE:
Tumeona aina za malaika mbalimbali na kazi zao, lakini kuna
huyu malaika wa Tatu ambaye ndio kerubi afunikaye, ambaye ni shetani . shetani
kabla ya kuasi alikuwa malaika wa mkuu kwenye ngazi ya kerubi, ambaye kazi yake
kubwa ilikuwa kufunika na ilikuwa kama eneo lina uharibifu akifika yeye aliweza
kufunika na kulifanya liwe takatifu mbele za Mungu.
Lakini baada ya kuasi shetani bado anaouwezo ule na
anautumia kuharibu maisha ya watu. kimsingi maisha ya mtu yanaweza kutafsiriwa
kirahisi kwa kutumia nyota. Kwahiyo kwakuwa shetani yupo rohoni anaweza kuona
viashiria hivi vya rohoni na kwa njia hiyo anatumia uweza wake wa kufunika
kufunika viashiria hivi na kufanya matokeo yake yanakuja kuonekana katika
mwili.
Nyota ni nini basi? Nyota ni kile kiashiria cha rohoni
kinachoonyesha eneo ambalo Mungu amekubarikia katika ulimwengu waroho. Kimsingi
kila mtu aliye duniani amepewa kitu na MUNGU
ambacho kwa hicho anaweza kukitumia ili afanikiwe kwenye maisha.mfano
nyota ya mtu yaweza kuwa ni akili au macho au mikono n.k.
Wachawi kwa kuwa ni watumishi wa shetani wanauwezo wa kusoma
nyota na kujua nini ambacho nyota inamaanisha. Hivyo kwa njia hii wanatumia
kuiba au kiufunika . akichukua nyota anaenda kumpandia mtu mwingine. Kwahiyo
shetani anaweza kufunika, na ndio maana wasoma nyota na wasafisha nyota
wanachofanya ni kuiba au kufunika nyota na kumpa mwingine anayehitaji kwa
wakati huo. Kuna watu wanaotumia nyota za watu kuendesha maisha ya watu..
Kuna watu wanaishi kwa kutumia nyota za watu, na kwa mamlaka
tuliyopewa tunaweza kurudisha kwa Jina La Yesu. Tumia mamlaka hiyo kurudisha
vyote LUKA 10:19 Tuna mamlaka ya kurudisha. Unaamuru kwa Jina la Yesu nyota
yako irudi kabisa. Mtu aliyechukua nyota yako anaweza kuwa wa karibu sana.
Maana adui wa mtu ni wa karibu ya huyo mtu ndugu au jirani.. lakini tuna mamlaka
dhidi yao wote amuru warudishe, nyota haiombwi bali unaamuru irudishwe.
Hatumwombi shetani bali tuna mwamuru.MUNGU akubariki sana By ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA

Comments