KWANINI TUNAFANYA MAOMBI?.MUNGU AMETUAGIZA TUOMBE

Mungu  mwenyewe ametuagiza tuombe.
Hakika Baba aliye na upendo anataka kushirikiana na watoto wake kwa njia ya maombi. Ushirikiano wa kuwasiliana  kati ya roho zetu na Mungu. Anatuhimiza mara kwa mara kufanya hivyo. Na huu ni uamuzi wa Mungu mtakatifu  kwamba tunaukuza ufalme wake, ni uchaguzi wake muhimu tunaoufanya kuliko kazi nyingine yoyote anatutumia, anatuongoza kuomba vizuri.

1Tim:2:1-3 "Basi kabla ya mambo yote nataka dua, na sala, na maombezi na shukurani, zifanyike  kwa ajili ya watu wote, kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri nalo linakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu."

Kwa maneno hayo tunaona  kwamba Mungu ameagiza. Tunaweza kusema kwamba Mungu ametoa amri. Tukiangalia  neno hili 'NATAKA' halina mjadala,  Yeye ndiye aliye juu ya vyote, ni wa kwanza kuliko vyote, Yeye anataka maombi yafanyike. Kwa maneno mengine tunaweza kusema kukosa kuomba ni dhambi, ni kosa la  kutokutii  agizo la Mungu, kama  Maandiko matakatifu yanavyosema  katika  1 Samweli 12 :23a
"Walakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi."  Dhambi hii ni mbaya na inaleta kizuizi. Hakuna jambo lolote litakalofanyika tusipoomba yaani  hakutakuwepo na maemdeleo yoyote. Tusizuie makusudi ya Mungu anayotaka kuyatenda; tutambue kwamba Mungu ni mwenye Busara kuliko sisi tulivyo, na  tukubali kuwa makusudi yake ni makubwa sana kuliko yetu.

2 Nyakati 16: 9 "Kwa maana macho ya BWANA hukimbia–kimbia duniani mwote ili ajionyeshe mwenye  nguvu kwa ajili ya hao waliokamilika moyo kuelekea kwake."

Lengo kubwa la Mungu ni kwamba anataka kuwa pamoja nasisi katika yote tunayohangaika nayo kila siku. Anataka kutusaidia hata katika kazi zetu za mikono. Hivyo anajitoa kabisa kwa ajili yetu akitaka kushirikiana nasi katika mambo yote.

Bila shaka utazidi kujifunza kuwa maombi ni msingi mkuu  wa  kazi  nyingine zote katika ufalme wa Mungu, ndio maana Mungu hatulii anataka watu waombe. Kama maandiko matakatifu yanavyosema katika kile kitabu cha Mathayo 7:7 "Ombeni nanyi mtapewa tafuteni nanyi mtaona bisheni nayi mtafunguliwa."
(a) Omba uweze Kupokea
(b) Tafuta uweze  kupata.
(c) Bisha mlango uweze kufunguliwa
 
Isaya 55 "Mtafuteni BWANA maadamu anapatikana mwiteni maadamu yu karibu."
Luka 18:1 "Akawaambia mfano ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu siku zote wala msikate
tamaa." Kufuatana na umuhimu uliopo katika kuomba hatupaswi kukata tamaa.


Wafilipi 4:6 "Msijisumbue kwa neno lolote bali katika kila neno kwa kusali pamoja na kushukuru na haja zenu na zijulikane na Mungu." Mungu anajua kuwa kuna mambo yanayosumbua, hivyo basi Yeye anatukaribisha kwake akisema yaleteni kwangu, hata mambo  madogo madogo nitawasaidia..
 
Sisi tunamhitaji Mungu kwa haja zote, tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, na katika yeye tunaweza kuendelea vizuri, vinginevyo tunaweza kupotea kabisa. Neno la Mungu linasema hivi katika Yohana    15:5-7 "Mimi ni mzabibu nayi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya  neno lolote. Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa."

Jinsi tunavyoendelea kuishi kwa kutambua na kutenda  jambo hili zaidi na zaidi, ndivyo tunavyozidi kumpatia Bwana  heshima..MUNGU awabariki sana

Comments