![]() |
EPHRAIM AKIWA NA MKEWE FAITH CHELISHE |
Ephraim
Sekeleti Mutalange ni muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Zambia,
alizaliwa Mwaka 1983 katika mji wa Kalulushi nchini Zambia. Alimaliza elimu
yake ya sekondari katika shule ya Kalulushi mwaka 2001.
Ephraim
ni mtoto wa pili toka mwisho kati ya watoto sita, aliingia kwenye muziki wa
injili tangu akiwa kinda huku alifundishwa kupiga kinanda na mmishonari
alipokuwa bado mdogo. Mama yake anasema “ Ephraim alikuwa ni mtoto
aliyekuwa wa kelele nyingi”. Yeye pamoja na dada zake waliimba kanisani
wakitumia kinanda na huko alipata uzoefu katika uimbaji na upigaji wa kinanda.
Baadaye alijiendeleza katika uimbaji kwenye kikundi kilichojulikana kwa jina la
“Virtue for Christ” na aliimba katika kikundi hicho kwa muda wa miaka
miwili.
Mwaka
2002 akiwa na kiu ya kurekodi album yake, Aliamua kujitoa muhanga kwenda Afrika
ya Kusini kwa kutumia kiasi kidogo tu cha pesa alichokuwa nacho, nia ilikua ni
kurekodi album yake ya kwanza. Pamoja na jitihada hizo, baada ya kufika nchini
Afrika ya Kusini alijikuta anaweza kurekodi nyimbo mbili tu kati ya album
nzima. Hivyo akaamua kujiingiza katika Theater ya Pretoria na ndipo akapata
fursa ya kuimba mbele ya Rais wa Afrika ya Kusini. Nafasi nyingi ziliendelea
kujitokeza zilizomsababishia kutaka kuacha kuendelea na muziki wa injili ili
aimbe miziki ya kidunia, lakini akawa muaminifu kuendelea na uimbaji wa injili.
Mlango ulifunguka kumruhusu kurekodi album ya kwanza iitwayo Temba Baby“(Mtoto
wa Miujiza)”.
Baada
ya kurekodi, na kuuza nakala za kutosha za album hiyo ya Temba boy, kwa
mafanikio ya hiyo kazi Ephraim aliamua kurudi nyumbani kuwekeza ile fedha.
aliona awekeze zaidi kwenye ya album yake ya pili iliyopata mafanikio makubwa
iliyoitwa Limo Ndanaka. Hi album imefanya vizuri kwenye chati mbalibali za
muziki wa injili. Ephraim akiwa nje ya Zambia ameimba katika nchi mbali mbali
zikiwemo Namibia, Afrika ya Kusini, Tanzania, Zimbawe na Australia.
Comments