NDUGU ZANGU WOTE 11 WALIKUFA MBELE YANGU TENA KWA SIKU MOJA



Naitwa Paulo Minani nimezaliwa mwaka 1968 huko mkoani Muyinga nchini Burundi katika familia ya watoto 6 na mimi nikiwa ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya mzee  Minani Rukara na mama Pendo Ruguge, katika familia yetu tumezaliwa watoto 6 na mimi nikiwa ni wa kwanza kuzaliwa kama nilivyosema na wengine ni wadogo zangu wa kiume 3 ambao ni Kasase, Baramba na Misago na dada zangu walikua ni Penina na Puli tumeishi vizuri tangu tukiwa wadogo hadi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini kwetu ambavyo kipindi vinaanza mimi nilikua nimeenda kumtembelea shangazi huko bujumbura karibu na mto Ruzizi lakini kwa sababu ya hali hiyo ya vita baada ya kifo cha Raisi Ndadaye nilirudi nyumbani muyinga na kuishi na wazazi na ndugu zangu lakini katika hali ya hofu na wakati vita vinaanza nilikua na mika 25 ila nilikua nimeshaoa ila nilikua sijazaa mtoto. Nakumbuka ilikua ni siku ya alhamisi na ikiwa ni wiki 3 tangu nitoke Mto ruzizi kwa shangazi vita vilikua ni vikali sana katika maeneo yetu na sitasema kabila langu ila ni moja kati ya makabila 3 makubwa katika nchi yetu yaani wahutu, watusi na watwa na katika eneo la kijiji chetu watu wa kabila letu walikua ni wengi sana na ndio waliokua wanatafutwa kuuawa. siku hiyo ya alhamisi nilikua sina amani na nilikua nimezunguka sehemu mbalimbali ili kama mambo yakiharibika tupate shemu ya kukimbilia mimi na familia yetu maana baba alikua ni mlemavu wa mguu hivyo kwa kiasi fulani walinitegemea sana na ilipofika saa 11 jioni nilirudi nyumbani na kuwakuta mama, baba, mkewangu na ndugu zangu 5 wamesimama nje ya nyumba zetu na wakaniambia kuwa katika kijiji jirani watu wengi wamekufa kwa sababu ya vita na wakaniuliza kama nimepata sehemu ya kukimbilia ili tupate mpenyo wa kutorokea Tanzania nikawambia nimepata na itabidi tutembee umbali mrefu hadi kijiji cha Kobelo ambacho kiko mpakani mwa Tanzania na Burundi na baada ya hapo tuombe majeshi ya Tanzania ambao walikua wanalinda mipaka yao watupeleke kwenye kambi la wakimbizi lolote huko Tanzania.  tulipanga kesho yake tungeondoka lakini tukio la ajabu sana ilitokea masaa machache sana baada ya kuwambia hivyo maana ilipofika saa 1 na nusu jioni yaani kama saa moja tu na nusu tangu niwaambie habari za kuondoka huko kesho yake, niliona nyumba zaidi ya 30 zikiungua na moto na nyumba hizi zilikua za majirani maana nyumba karibu zote katika maeneo hayo zilikua za nyasi hivyo ilikua ni rahisi sana kuungua. kwa haraka sana niliwakusanya ndugu zangu wote pamoja na watoto 3 wa ndugu zetu wengine katika ukoo ambao walikua wanaishi jirani na kwetu lakini nilikua nimechelewa sana kumbe hawa jamaa wauaji walikua wanachoma moto nyumba kama tano huko wakiwa pia wamezingira nyumba kama 7  za mbele hivyo tulikua tumezingirwa muda mrefu bila kujua, Watu hawa walidhani mimi ni mwanajeshi hivyo nlikua natorosha ndugu zangu ili wanajeshi wenzangu wa jeshi la serikali waje kuwaua wao hivyo walidhani mimi ni mwanajeshi na nilikua huko kiupelelezi na ili kuwaondoa ndugu zangu kumbe walikosea maana sikuwa mwanajeshi na mambo ya kijeshi wala sifahamu hata moja. wakanifunga kamba mikononi na kusema mimi wataniua baadae ili kwanza niwaeleze habari za jeshi la taifa na wale ndugu zangu wakiwemo baba, mama, mkewangu, wadogo zangu 5 na ndugu wengine 3 walianza kuuawa. Ndugu ukiona uko mzma fulani mara mia zaidi na hakika tunaishi kwa neema tu ya MUNGU na hatuna cha kumlipa hata kimoja kwa kile ambacho ametenda kwetu kwa kutupa uzima. walianza kwa kumwua dada yangu Penina wakidhani kuwa ni mke wangu walimkata mkono na matiti na kumkata kwa panga shingoni akafa huku nashuhudia baada ya dada yangu walimchoma singe baba na mama na singe hizo a bunduki walichoma kutokea sikio moja hadi jingine  huku nikishuhudia na kiukweli nianza kuhisi kizunguzungu. baada ya hapo walimwua mke wangu kwa kuchoma mkuki na na kumkatakata miguu na mikono na sidhani kama kuna watu makatili kama hawa katika hii dunia na kumbuka haya matukio ya kuuawa kwa ndugu zangu ndio matukio ya kwanza mimi kuona mtu akiuawa na nasema haya kwako leo ni kama tu niko sawa lakini nikikumbuka huwa nalia sana na inaumiza sana na kama sikufa kwa ugonjwa wa moyo siku hiyo basi sitaugua ugonjwa wa moyo tena maana moyo uliuma kuliko kawaida na waliendelea kuua mmoja mmoja hadi wote kumi na moja na tukio baya zaidi ni kuwatoboa kwa singe kutoka sikio moja hadi jingine ili wahakikishe kama wamekufa baada ya hapo nilikua siwezi hata kuongea. Ndugu nakuambia hata sasa mtukuze MUNGU maadamu ungali hai na furahia ukombozi wa BWANA YESU maadamu umepewa nafasi ya kuishi. Baada ya hapo nilichukuliwa na kuunganisha na watu kadhaa ambao waasi walisema ni wanajeshi waliotekwa na tukawa kama 20 na tukapandisha kwenye gari na kupelekwa Mkoa wa Ngozi kwenye pori ambalo lilikua ndio kitua chao cha mateso ya wanajeshi waliowakamata ili kuwapa mateso watoe siri zote ili iwe rahisi kwao kuchukua nchi. Tulipokaribia kufika tulifungwa vitambaa kichwani ili tusifahamu tulikopelekwa na baada kama ya nusu saa tulifikishwa na kufungwa kwenye miti sehemu moja na kuanza kuambiwa ili tuwe salama tutoe siri zote za serikali na kiukweli wenzangu baadhi yao walikua wanajeshi lakini mimi sikujua lolote na namshukuru MUNGU sikuongea chochote maana akili yangu ilikua kama imeganda nikikumbuka vifo vya ndugu zangu. tuliteswa sana na  wengi walisema mengi sana kuhusu serikali na viongozi wake waliko  na kesho yake ilikua tuuawe maana wao hawana chakula cha kutupa hivyo tutoe siri na tuuawe na kesho yake alikua anakuja mkubwa wao mmoja wale waliotuteka hivyo walisubiri akija atuhoji na baada ya kutuhoji watuue,  usiku huo huo mmoja kati ya mateka wenzetu ambaye alikua ni mwanajeshi aliona bomu lililokuwa limewekwa chini yake ili akikata kamba aangukie bomu na kufa pamoja na sisi lakini huyu jamaa alituambia usiku tukiwa na njaa kali kwamba yeye yuko yayari kufa hivyo tufanye mbinu ya kumfungua na tulifanya kazi ya ziada kumfungua mmoja wetu ambaye alimfungua huyo jamaa maana wale walinzi walijua tuna siku mbili hatujala na wametupiga sana hivyo tusingetoroka. lakini zoezi lilifanikiwa na tukamfungua na sisi wote kufunguliwa na kwa sababu eneo hilo walipanda mabomu jamaa alituambia kuwa kusuiri hapo hapo tukiwa tunajifanya tumefungwa kamba na ilipofika sana 12 asubuhi wale walinzi walikua na kutukuta tumetulia tu na wakati wanasogea yule mwanajeshi alitupa ishara akashika lile bomu na kulilipua na wakati huo huo nikaanguka chini na kuamka nikiwa salama na kuanza kukimbia ila nilichokua nasikia nyuma ni risasi yaani wale watekaji walitekwa wao na najua waliuawa na wale jamaa wenzangu waliondoka eneo lile lakini yule shujaa wetu alikufa na baada hapo nilikimbia na kuanza kula matunda matunda fulani maarufu kwa jina la Makome, Nilipata nguvu kidogo na baada ya siku tatu nilikua mto kagera mpakani mwa Tanzania na burundi ambapo niliona mizoga mingi ya watu ambao kwa hofu walitaka kuvuka mto lakini walianguka maana maeneo hayo maji yanaenda kasi sana hivyo sio rahisi kuvuka kama hujui kuogelea . nilifanikiwa kuvuka na kukamatwa na majeshi ya Tanzania na kuunganishwa kwenye magari ya UN na kupelewa Rusumo Ngara kwenye kambi ya wakimbizi na baadae kwa ufupi ni kwamba nilikaa kwenye kambi ya wakimbizi kwa miezi 5 na baadae nilitoroka kwa sababu ya idadi kuwa kubwa sana ya wakimbizi kiasi kwamba walinzi walizidiwa na nilitolokea Biharamulo katika kijiji cha Choga na baadae niiishi nyabusozi na sasa niko Mleba na nimeshachukua uraia wa Tanzania, Nimeokoka na nina hubiri injili ya BWANA wetu YESU KRISTO, namshkuru MUNGU kwa kunipa nafasi ya kuishi na kwa nafasi hiyo ya uzima alionipa nitamtumikia siku zote za maisha yangu kwa sasa japokua naelekea uzee maana na miaka 45 lakini nimejaaliwa kuona na kuzaa watoto 2 na wote tupo kwa ajili ya YESU ili kuhubiri habari njema za ufalme wa MUNGU ambapo hakuna uzima kwingine nje na YESU. MUNGU BABA wa mbinguni awabariki sana

Comments