NILILALA NA PAKA NA AKAGEUKA NYOKA KITANDANI KWANGU



MSAADA WA KWELI NI YESU KRISTO

Ndugu wapendwa tuanaishi katika dunia iliyojaa kila aina maovu na uonevu mwingi sana. wakati mwingine tunatafuta msaada kwa wanadamu lakini msaada wa wanadamu ni wa muda tu na uongo ni mwingi sana. Naitwa John niko Arusha na ni mwenyeji wa hapa hapa Ungalimited Arusha. nina mika 31 na nimeoa na kujaaliwa kupata mtoto mmoja  pia nimeokoka tangu 2010. katika maisha yangu ya nyuma kabla ya wokovu niliteswa sana na nguvu za giza na ilifika kipindi cha kukata tamaa  yapo memgi sana yaliyonitokea lakini hili la kulala na paka hua mpaka sasa nikikumbuka nasisimka nywele japokua nafahamu kwa sasa siwezi kuchezewa na uchawi tena maana YESU niliyenaye amenishindia na atanishindia milele. Ilikua nov 2008  ilikua siku ya jumatano nilienda kuangalia mpira UEFA na nilirudi mida ya saa 5 usiku na nilipofika nilipokua nimepanga niliingia ngani na kuwasha taa hakukuwa na kitu na baadae nikafunga net na kulala ilipofika saa 10 alifajiri nilijikuta nasikia joto maeneo ya kifuani na kuanza kupapasa labda ni mto wa kuegemea kichwa ulikua umekaa pale na nilipoanza kupapasa niligusa manyoya na nlipozidi kupapasa nilizidi kugusa manyoya kitendo kilichosababisha kuamka kwa nguvu na kutoka ndani ya chandarua haraka huku nikiogopa sana . nilipotoka niliwasha taa na kumwona paka mkubwa sana mweusi ambaye hata sijui ameingiaje chumbani kwangu maana hakuna sehemu ya kupitia paka kama huyo pili ameingiaje ndani ya kitanda maana kuna net nafunga yaani hata iweje paka kama huyo katika mazingira ya kawaidi hawezi kuingia kwenye chandarua tatu ameingiaje kwenye shuka na kulala tena kujinyoosha kama binadamu nne kajifunika shuka langu je ana akili za kuchukua shuka na kujifunika?. Haikua kawaida ni nguvu za giza sasa nikaanza kuwaza kwamba ni nani anayenichezea hivyo na nilitafakari ni nani ni adui yangu au ni nani tumekosana siku za karibuni hata akaanza kunifanyia hivyo? Nilifungua mlango na kutoka nje maana yule paka niliogopa hata kumfukuza maana ni mkubwa na anatisha yaani ukubwa wake ni kama chui saizi ya kati. nilizunguka nyuma  na kuanza kuchungulia dirishani na baada ya kama dakika 8 yule paka aligeuka na kuwa nyoka na baada ya muda kidogo yule nyoka akawa anatoa mwanga japokua taa ilikua inawaka lakini yeye alitoa mwanga kama wa moto na baada ya muda kidogo akatoweka. Sikuingia ndani ya chumba changu hata saa 6 mchana na kwa tukio hilo la siku moja nilijikuta  nawachukia watu sana na kuanzia muda huo moyoni mwangu  kila mpangaji mwenzangu nilimchukia na nakumbuka kulipokucha nikiwa nimejiinamia nje kwa kuogopa kuingia ndani kuna mama wa jirani alipita na kunisalimia kwa nia nzuri tu lakini kwa sababu ya taharuki moyoni mwangu nilimjibu kwamba  nitamkatakata kwa mapanga kwa tabia yake ya uchawi. yule mama alikodoa macho na kunishangaa na kusema uchawi upi tena? akasema yeye hahusiki na uchawi na hawezi kuroga maana mambo hayo hayajui hata kidogo tena akasema nimwombe msamaha nilikataa maana nilihisi kwamba kihelehele chake cha kunisalimia wa kwanza ndicho kilichosababisha nimwambie vile kumbe ni kiwewe tu cha tukio la jana sikukaa kwa amani hata kidogo maana nilishuhudia kwa macho yangu jinsi paka alivyogeuka nyoka na kwa wiki nzima sikulala kwa amani na muda mwingi nililala mchana tena kwenye chumba cha rafiki yangu ambaye nilikua naenda kumtembela au kupiga story na nikifika tunaongea kidogo harafu nalala na kuna siku aliniuliza je usiku nalala wapi nikicheka tu na kumwambia  nilikua nalala kwa girlfriend wangu kumbe haikua kweli . baada ya wiki mbili nilianza kurudi kwenye hali ya kawaida na kuanza kulala ghetoni kwangu kama kawaida na hakukua na tatizo lile tena lakini baada kama ya mwezi mmoja kupita na nakumbuka siku hiyo ilikua siku ya jumamosi ni siku ambayo sitaisahau na ndio chanzo cha kukuandikia habari hii nililala  na ilipofika kama saa 8 usiku nilijigeuza katika hali ya usingizi na kugusana na kitu kiguma kilefu kama binadamu tena kizima maana joto kama la mtu nililisikia. nikaruka ghafla hadi net ikakatika nikakimbila mlango ili nitoke nje lakini niliukoswa na kiukweli siku hiyo nilijinyea kabisa na hata sikujuia kinyesi kilitoka vipi lakini nilikuja tu kukuta nina mavi kuanzia kiunoni hadi miguuni na kilichoendelea baada ya hapo kuna kama mtu alinyanyuka kitandani na kuja kuwasha taa mawazo yangu yote nilimwazia paka wa siku ile. Baada  ya kuwashwa kwa taa nilimwona msichana  ambaye aliniambia kuwa siwezi kumkimbia hata siku moja aliniambia haraka nirudi kitandani na kulala maana hakujakucha. kwa leo ni kama inachekesha lakini siku hiyo ilikua ni hatari kuliko hatari zote maishani mwangu  nilirudi kitandani  na yule dada aliyekua amevaa kimini aliniambia kwamba nilale na kuniambia tena kwamba tungefanya mapenzi ila mimi ni mchafu ninanuka mavi. sikujibu neno hata moja maana kwa muda huo nilihisi kufakufa. sikusinzia na yeye alikaa kwenye kiti na baada ya muda kidogo nilisikia kicheko na nlipochungulia niliona paka wa siku ili yaani yule binti wa kimini kageuka paka niliruka tena  hadi chini na yule paka akaanza kuongea kama mwanadamu huku akinitukana kwamba sana kwa uchafu wa kinyesi na baada ya hapo alisema atakua anakuja kunitembelea maana amenipenda tena kwa miaka 10. Sikujibu kitu na muda kidogo aligeuka na kuwa binadamu tena na akatoweka ghafla. Sasa nilijua kilichokua kinaendela na kesho yake bila kuaga niliondoka na kuelekea singida nikiwa nimepanda basi la kuelekea mwanza tulifika salama na nikaenda kulala kulala gest pale singida  na lengo langu kesho yake nitafute makao mapya maana nilikua na pesa kidogo kama laki 9. Nikiwa nimelala usiku yule dada alinitokea tena na kuniambia kua siwezi kumkimbia hata siku moja na kwa taarifa yangu ni kwamba tumesafiri wote ndani ya basi tena alikua amekaa jirani na mimi ila hakujionyesha kwangu ili nisishtuke na kujinyea mbele za watu. sikujibu neno lolote  na napenda kukuambia mtumishi kuwa baada ya pale yaliendelea matukio mengi tu na nikakimbilia Dar lakini ndio kwanza yule dada aliendelea kunisumbua na umbo lake la paka lakini mambo hayo ndio yakawa chanzo cha mimi kuokoka na tangu siku nimeombewa na kumkiri YESU KRISTO kuwa ni BWANA na MWOKOZI wa maisha yangu mwaka 2010 mambo haya hayajatokea tena na siku naombewa pale Sinza ilisikika tu sauti ya yule dada akisema ipo siku tu ataninasa na kuniua maana yeye na ndugu zake wameungua na moto mbaya uliotoka hapo kanisani.Hawezi tena milelel na hua najiuliza ilikuaje hata kuanza kunisumbua mimi na ilikaribia mimi kujeruhi watu kisa hili li mzimu tena muda mwingine akiongea kwa kejeli na kicheko huku akinicheka kwamba nitajinyea?. Hata hivyo kuna baraka katika KRISTO maana mwaka 2011 mwishoni nilifunga ndoa kule kule arusha ambako naishi sasa na tuna mtoto mwenye miezi 7. Namshukuru sana MUNGU na hakika katika YESU tunashinda na zaidi ya kushinda,

Comments