Kwanza kabisa nataka nimshukuru mungu kwa
kuniokoa,asingekuwa huyu yesu sijui leo ningekuwa wapi hakika mungu yupo
kama huamini kupitia hili la kwangu amini yupo,mimi ni msichana naitwa
N.ilikuwa siku ya alhamisi ambapo nilienda nyumbani kuwasalimia wazazi
wangu nilipofika nyumbani nilimkuta dada yangu ambaye tumezaliwa pamoja
amerudi nyumbani kwani yeye ni mganga hakuwepo nyumbani mda ,alinipokea
kwa furaha ila sikujua nafsi yake iliwaza nini juu yangu siku ya pili
nikamwambia mama ngoja twende na dada sokoni tukaondoka kama kawaida
tulipofika njiani dada yangu aliniambia nimpeleke kuna mahali kuna babu
mmoja nataka kwenda kumuona nikamkubalia tukaenda tulipofika huko yule
babu nilishangaa akimukaribisha kwa furaha kubwa na kumwambia huyu ni
ndugu yako ameshakuja akasema ndio kumbe sikujua kama kuna kitu
kinaendelea kati yao ,wakatukaribisha ndani baadae nikaona dada yangu
akipewa maji kidogo anywe ,nikaona amekunywa
pia wakanipatia na mimi kidogo na kuniambia ukinywa maji hayo utaona
wachawi wako ote nikawambia sipo tayari dada alinishawishi sana hadi
nikakubali na ndio ulikuwa mwanzo wangu wa kupoteza faham na kujikuta
nipo kwenye chumba cha giza nikiona kama watu wamelala uchi ila hawawezi
kusema nilitamani kuongea lakini faham zangu zilifubwa ila niliweza tu
kuona yanayoendelea baada ya hapo nilimuona dada yangu yuko pembeni
akining'onga ila yeye hakujua kama mimi faham zangu zilikuwa
hazijapotea sana ndipo nikasikia sauti ndani ya hiyo nyumba kuwa unaweza
kurudi au kutokurudi ufaham wako ndipo sikujua kabisa chochote ila
nilichokumbuka nilikuwa na simu mkononi kuna wimbo huwa napenda ulikuwa
kwenye simu mara zote huwa nausikiri ni wimbo unaosema yu mwamba yesu"
nilijikuta nimeponyeza na ukaanza kulia pale pale faham zangu
zikanirudia na kujitambua dada yangu aliogopa sana nikamwambia tuondoke
nilipofika mjini sijui aliambiwa anipake dawa hafu aniache mjini niwe
kichaa alifanya hivyo nami nilikuwa tayari nishajua yote aliponipaka tu
nikasema ninahari vyote kwa damu ya yesu hakika nilimuona dada yangu
akiondoka mbele yangu na kuniacha mjini nikiwa natangatanga baadaye
nilipata faham nikaenda nyumbani nilipo fika nyumbani nilimkuta yupo
sikusema jambo ila nilimwogopa sana na nilijikuta nikitapika vitu vyote
nilivyolishwa hakika Mungu ameniokoa nampenda na nitamuhimidi siku zote
amen
Comments