SIFA ZA MUNGU TUNAYEMWOMBA

JOHNSTONE SUNDAY MOSHI
SIFA ZA MUNGU TUNAYEMUOMBA:-
1=>MUNGU ANAISHI : zab 90:2 "kabla haijazaliwa milima,wala hajaiumba dunia,na tangu milele hata milele ndiwe MUNGU" ..MUNGU yeye alikuwepo kabla hata ya kitu chochote,hazeeki kama mwanadamu unayeishi duniani wala kufa,
Waebrania 1:10-12 "Na tena wewe,BWANA hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi,na Mbingu ni kazi za mikono yako,Hizo zitaharibika,bali wewe unadumu..Nazo zote zitachakaa kama Nguo"
2=>MUNGU NI MWEZA
Mwanzo 18:14.."Kuna neno gani lililogumu la kumshinda BWANA"
->Sisi wanadamu ni Dhaifu
->kuna vitu vingi tunashindwa kufanya kwa akili wala Nguvu zetu..
*Kwa uweza mkubwa wa MUNGU aliumba mbingu na nchi kwa nguvu na uweza wake..
3=>MUNGU HABADILIKI -yeye ndiye mwanzo na tena mwisho,yeye ndiye alpha na tena ndiye Omega,kila kitu katika dunia hubadilika mavazi,vyakula,maisha,afya,ukuaji lakini MUNGU HABADILIKI..
->MUNGU aishie habadiliki leo wala kesho kwani ni MUNGU ASIYEBADILIKA
Malaki 3:6 "kwa kuwa mimi BWANA sina kigeugeu(sibadilikibadiliki) ndio maana ninyi hamkuangamizwa,enyi wana wa Yakobo"
4=>MUNGU NI ROHO
->MUNGU siyo mwanadamu kama mimi na wewe tulivyo...YOH 4:24 "MUNGU ni ROHO,nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli"
Mungu hana madhaifu wala magonjwa ya mwili kama tulivyo sisi wanadamu
luka 24:39 "Tazameni mikono yangu na miguu yangu,ya kuwa ni mimi mwenyewe,nishikenishikeni,mwone kwa kuwa ROHO HAINA MWILI NA MIFUPA KAMA MNAVYONIONA MIM KUWA NAYO..
5=>MUNGU NI NURU : Yoh 1:5 "Nayo NURU ya ng'aa gizani,wala giza halikuiweza"
6=>MUNGU NI UPENDO 1YOH 4:8 "Yeye asiyependa,hakumjua MUNGU kwa maana MUNGU NI UPENDO"
=MUNGU alitupenda,alionyesha upendo wake mkuu kwa ajili yetu kwakumtoa mwana wa pendo lake,mwanae kipenzi,mwana wake wa pekee kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu tupate kuwa huru
1Yoh 4:10 "Hili ndilo pendo ,si kwamba sisi tulimpenda MUNGU,bali kwamba yeye alitupenda sisi akamtuma mwanawe(YESU) kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu" Hata sasa MUNGU anatupenda na mkimfuata yeye mmepata vyote. MUNGU awabariki sana ni mimi mwinjilisti

JOHNSTONE SUNDAY MOSHI

Comments