TUNAOMBA ILI TUISHI MAISHA MATAKATIFU

Tunaomba ili tuishi maisha ya utakatifu.
Wakati tunapokosa au tunapomkosea Mungu kwa kutenda dhambi, kwanza kabisa tunapaswa kujua kwamba Mungu anatuona, na anajua nini tumefanya, hatuwezi kujificha mbele za Mungu. Hivyo kwa sababu Yeye  anatupenda na anataka kutusamehe, anataka tuungame dhambi zetu. Hapendi  tuendelee kubaki katika hali ya dhambi. Kwa hiyo hatupaswi kukaa kimya ikiwa tumekosea. Tunatakiwa tunyenyekee na kujieleza kwa  kusema wazi mbele zake yale tuliyotenda. Katika kitabu cha Yeremia  8:6 Neno la Mungu linasema: "Nalisikiliza nikasikia, lakini walisema yasiyo sawa; hapana mtu aliyetubia maovu yake, akisema, nimefanya nini?..."

Na katika Yohana 1:9 imeandikwa: "Tukiziungama dhambi zetu yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote."

Maombi hutusaidia ili tuweze kutakaswa, tuweze  kusafishwa. Hivyo inatupasa  kuungama na kutubu dhambi zetu. Tunatakiwa tujue kwamba tukikaa katika dhambi hatutahesabiwa haki mbele za Mungu. Mungu anataka kutusaidia tushinde dhambi na kuishi maisha ya utakatifu. Yak:5:16a "Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa."
2 Nyakati 7:14 "Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuacha njia zao mbaya; basi nitasikia kutoka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.".MUNGU awabariki sana

Comments