KATIKA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI TUJIFUNZE HABARI ZA DEBORA


Leo tarehe 08 march 2013 ni siku ya wanawake duniani {WOMEN'S DA} na katika kujifunza  au kujua jinsi MUNGU anavyowatazama wanawake lazima tuangalie kwenye BIBLIA maana kwa MUNGU watu wote ni sawa  na MUNGU hana upendeleo na kwa sababu hiyo MUNGU alimchagua Debora katika madaraka makubwa zaidi katika taifa la Israel na ingekuwa leo basi huyu mwanamke alikua ni kama Raisi wa nchi maana hakukuwa na kiongozi mkubwa zaidi yake katika waisrael wote enzi zile na kwa taifa la Israel Debora alikuwa ni kiongozi wa mkuu wa kiserikali na kiongozi nkuu wa kiroho maana yeye ndio alikua anapokea ujumbe kutoka kwa MUNGU kwa kwa taifa zima yaani alikua ni mwamuzi, karibu tujifunze

Baada ya kifo cha Joshua aliyewaongoza wana wa Israeli kuingia nchi ya ahadi ya Kanaani, Mungu aliwainua waamuzi kuwaongoza wana wa Israeli. Miongoni mwa waamuzi hao alikuwepo mwamuzi wa kwanza na pekee wa kike aitwaye Debora. Debora aliwaongoza wana wa Israeli kwa ujasri mkubwa na aliheshimika sana na watu wa nchi yake. Biblia inatuambia kuwa Debora alikuwa ameolewa  na hilo halikumzuia kufanya  majukumu yake kama mwamuzi kwa ufanisi.

Waamuzi 4:4-5 “Basi Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule. Naye akakaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israel ” wakakwea kwake, awaamue.

Ndoa haipaswi kukuzuia kufanya huduma yako bali inapaswa iwe mahali ambapo huduma yako itasaidiwa na kutiwa moyo.Debora pamoja na kuwa ni mwamuzi wa kwanza mwanamke  alitimiliza majukumu yote tena kwa ufanisi mkubwa na kuifanya Israeli kufanikiwa kuwaangamiza maadui wao waliowatesa kwa miaka mingi na hatimaye kuishi kwa amani kwa miaka arobaini.

    Alikuwa kiongozi wa taifa
    Aliwaamua katika matatizo yao mbalimbali
    Alikuwa nabii aliyewapa watu maagizo toka kwa Mungu
    Aliheshimika na watu wote


Mungu haangalii jinsia ya mtu bali anaangalia moyo ulio tayari kumtumikia na kuyafufuata makusudi yake. Barak, mkuu wa jeshi la Israel alijua kuwa Debora anakibali mbele za Mungu ndio maana alipotakiwa kwenda vitani alisema kama Debora hataambatana naye basi hatakwenda. Usijidharau sababu ni mwanamke na kuona kuwa huduma fulani ni za wanaume tu, hii si kweli mwanamke anaweza kuwa mwinjilisti, mchungaji, nabii, na pia nyadhifa za kiseriali. Mwanamke simama imara na songa mbele ukimpendeza MUNGU na wanadamu.
Mungu akubariki sana.

Comments