Posted by
Peter Mabula
- Get link
- X
- Other Apps
![]() |
Raphael GP Mbogo |
Dhambi-ni roho chafu/roho ya uasi ipingayo haki ya Mungu.
-hii dhambi(roho)ikitawala ndani yako itakufanya utende yale hukutaka
kwa hiari yako..itakufanya utii kila inachotaka na kila jambo
utakalolitii ni kinyume na Mungu.
-Roho ya dhambi hukaa ndani ya
mtu(Rumi 6:12 - Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;
)Paulo anawaambia Warumi dhambi isitawale NDANI ya miili
yenu,kwanini?-NI kwa sababu ikitawala utakuwa mfu kwa ajili ya kutii
sheria ya dhambi ambayo itakutenga na Mungu..
Roho ya dhambi ni roho inayotumikisha katika giza.(Rumi 7:15-16 - Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.
Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu
).
Dhambi sio sifa njema wala sio fasion,
Dhambi haikupi afya wala amani wala furaha bali majuto.
Nuru Ya YESU KRISTO itumulike sote tuone uzito wa dhambi tuzibebazo na MUNGU atuwezeshe kuishi maisha matakatifu yanayompendeza yeye siku zote. MUNGU awabariki sana. Ni mimi ndugu yako Raphael GP Mbogo
![]() |
Roho ya dhambi humtawala mtu na kumlazimisha kutenda uovu |
- Get link
- X
- Other Apps
Comments