HATUA TANO ZA MATUMIZI YA NENO LA MUNGU

Edward Tibenda


1.Omba kwa ajili ya ufahamu sahihi na matumizi mazuri ya kanuni za kiroho (Yakobo1:5 “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.”).

2.Fikiri sana juu ya sura unayoisoma. Hii hujumuisha pamoja na kushirikisha mistari mingine katika neno la Mungu katika sentensi, sentensi katika aya na aya katika sura na sura katika vitabu vingine. (2 Timotheo 2:15 “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.”).

3.Jaribu kuruhusu ufasiri wa kiroho toka katika sura hizo. Mara nyingi neno la Mungu hulandana hata katika mazinigra na tamaduni zake. Kwa mfano uzinzi (tendo la ndoa nje ya ndoa) hii ni dhambi katika mazingira na hata tamaduni za kibiblia. Kwa hiyo kusudi na wazo la Biblia uzinzi hautakiwi (Warumi 13:8-10 “Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.”).

4.Uaminifu ni kipimo chako kuona kama unatoka katika maandiko na kuhusisha upuuzi wako na maandiko. Hii huhusisha ufasiri mbaya sana mbele za Bwana (1 Yohana 1:9 “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.”) na hata mwenendo wa kiimani (Wakolosai 2:6 “Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye”). Wanafunzi itakuwa vizuri kusoma Zaburi ya 51 na wanakili mambo fulani toka katika toba ya Daudi aliyoifanya juu ya dhambi aliyoifanya kwa Bethsheba (2 Wakorintho 13:5 “Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa.”).

5.Tembea katika neema na Imani. Mtume Paulo anatuambia “basi kama mlivyompokea Yesu Kristo Bwana enendeni vivyo hivyo katika yeye.” (Wakolosai 2:6). Tumepokea kwa neema kwa njia ya imani (Waefeso 2:8-9 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.”) na hivyo hatuna budi kutenda matendo yanayolingana na neema tuliyoipokea. (Waefeso 2:10 “Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.”).  MUNGU awabariki. by

Edward Tibenda

Comments