JE WAFAHAMU NJIA ZA KUTOA UCHAFU KATIKA MIILI YETU ?

Mtumishi Gasper Madumla


Tuangalie njia tatu kati ya njia nyingi zilizopo ;

* MAPAFU

Kila kiumbe hai kinahitaji hewa ya oksijeni ili kiweze kuishi. Kila kiumbe kina namna ya kujipatia hewa hii muhimu kwa uhai. Kwa mfano samaki huipata kutoka majini kwa kutumia matamvua, mimea hutumia majani wakati wa usiku. Halikadhalika wanyama jamii ya mamalia hujipatia hewa kwa kutumia mapafu. Binadamu ana mapafu mawili yaliyo ndani ya kifua. Kwa maelezo zaidi kuhusu mapafu angalia mapafu.

Binadamu hutumia hewa ya oksijeni katika kujitengenezea nishati kutoka katika chakula kwa ajili ya matumizi mbalimbali mwilini. Miongoni ya matokeo ya pambano la chakula na oksijeni pamoja na vimeng’enyo mbalimbali ndani ya seli ya binadamu, pamoja na vitu vingine ni hewa ya carbondioxide. Hewa hii husafirishwa katika damu mpaka ndani ya mapafu ambao huitoa nje kama uchafu ndani ya mwili. Kiwango cha hewa ya carbondioxide kinachotolewa nje kila mtu anapopumua kinaweza kufikia asilimia nne au zaidi ya hewa yote inayotolewa nje. Zaidi ya hayo mapafu hutoa maji mengi kwa namna ya mvuke.

* INI

Ini ni miongoni mwa ogani muhimu katika mwili wa binadamu. Pia ini ni mojawapo ya viungo vinavyohusika katika kutoa uchafu. Ini hutumika pia katika uhifadhi wa chakula katika mwili wa binadamu. Chakula kinapofonjwa kuingia mwilini katika utumbo mwembamba huelekea kwanza katika ini. Ini husafisha sumu katika mwili. Kunapokuwa na uongezeko la chakula cha protini, ni jukumu la ini kurekebisha. Uchafu unaotolewa na ini huingizwa katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na hutolewa pamoja na kinyesi.
[hariri] Mfumo wa mkojo
[hariri] Mafigo

* FIGO

Katika mwili wa binadamu mafigo yamewekwa nyuma ya tumbo; moja kwa kila upande wa pingili za juu za kiuno. Sehemu ya juu ya mafigo imehifadhiwa kwa jozi mbili za mbavu zinazoelea. Kila figo kwa umbo lake hufanana na haragwe, lakini kwa ukubwa ni tofauti sana. Figo la kulia kwa kawaida ni fupi na nene zaidi, nalo, kwa sababu ya ini, hukaa chini zaidi kuliko figo la kushoto.

Mafigo yametengenezwa yawe mfano wa chombo cha kuchujia maji. Kazi yake ni kuchuja maji na kutoa uchafu na vitu vyote visivyohitajika mwilini vilivyochukuliwa na damu katika safari zake. Maji hayo pamoja na vitu hafifu vilivyomo ndiyo mkojo. Mafigo yameshehenezwa na vifereji vilivyonyongwanyongwa, navyo vyote huunganika pamoja kufanya bomba lile litokalo katika kila figo na kufika mpaka katika kibofu cha mkojo. Kutoka hukoo mkojo hutolewa nje kwa mshipa wa kupitia mkojo na uume/uke.

UBARIKIWE.

Comments