MUNGU ALIMTUMA MALAIKA ILI ALETE UPONYAJI KWANGU








AMOS OKELLO AKIWA NA MCHUNGAJI ELLY BRIGHTON BOTO WA KANISA LA KAWE PENTECOSTAL CHURH (KPC)
Mimi naitwa amos omela  nimezaliwa mkoa wa Shinyanga.  kunako mwaka 2012 mwezi wa kwanza niliugua tumbo nilienda Hospitali ya kijeshi ambayo ni Lugalo kwa ajili ya kupata matibabu nilifanikiwa kumuona Doctor akanifanyia kipimo cha Ultrasound pia akaniandikia nipime tena kipimo kingine kiitwacho X-ray kwa bahati mbaya naenda kufanya hicho kipimo umeme ukakatika na baada ya muda ukarudi akanipima tema na nikagundulika na tatizo la figo imevimba inafeli kusukuma mkojo akanipa rufaa ya kwenda Hospitali moja iitwayo Tmj kweli nikaenda kumuona Doctar nilifanikiwa kupiga X-ray doctor alisikitika nakusema ''pole sana kijana'' basi kwa maneno yale nikaingiwa na hofu nikakata tamaa nikajua nimekufa tayari paleple mchozi yakanitoka doctor akasema jipe moyo kuna dawa nitakupa utumie siku kumi ila nakuomba Muombe sana MUNGU akusaidie wewe ni mtoto mdogo sana kufanyiwa oppression  ya namna hii pia dawa za kukupa hazipo maana kwa sasa hizo dawa zimeisha na ili tukuagizie India unatakiwa ulipie Tsh. 60,000 nitakupigia simu baada ya siku mbili akanipa tahadhali kuwa hali ikibadilika niende Muhimbili akanipa barua ya zarula kweli nikafanya hivyo .Nikaondoka pale kuelekea nyumbani siku hiyo mvua ilikuwa inanyesha na kwa bahati nzuri nilikuwa na mwamvuli maana niliiona dalili mapema,wakati nasubiri gari kuna dada mmoja akatokea pale nilipo sijui alitokea wapi akaniomba nimkinge mwamvuli asije akaloana na mvua kweli nikamkinga akaniuliza kwanini huna amani nikasema dada acha tu maana sikutaka kila mtu nimuelezee matatizo yangu Yule dada hakukata tamaa kuniuliza tena mara ya pili nikamjibu nikamwambia kuwa ni ''matatizo ya dunia dada acha tu''  akaniambia naweza kukusaidia hata kwa mchango wa mawazo kaka mpaka nikaona kero, gari nazo haziji ikabidi ni mwambie ukweli uliopo kuwa dada mi naumwa figo akasema usiogope utapona tu kaka unak,a wapi hapa Dar nikamwambia nakaa kawe aniambia kuwa tamka mara kumi neno hili (KWA KUPIGWA KWAKE YESU SISI TUMEPONA)  kila siku kwa siku kumi alipo maliza tu kuniambia hivo gari likaja nikapanda sikujua kama na yeye alipanda gari au la nikakaa kusubiri kupigiwa simu nikachukue zile dawa kweli nilipigiwa nikaenda kuchukua doctor akanisisitiza tena kuwa muombe sana MUNGU asaidie hizi dawa kweli nikawa najuhudi kuomba kila ninapo taka kumeza naomba kwanza MUNGU kwamba atie nguvu hizo dawa nikisema pia 'Baba nakuomba nilifanya hivo mpaka siku kumi zikafika nikaenda kufanya checkup na niwe mzima.'' Baada ya siku 10  nikaenda Hospitali moja inaitwa IMTU sikufanikiwa kufanya vipimo vyovyote nikarudi nyumbani kesho yake nikaenda TMJ Hospitali bahati nzuri nikamkuta Yule doctor wa mwanzo akaniuliza vipi kijana unaendeleaje? nikamwambia afadhali kidogo na nimekuja kufanya check up nione naendeleaje akanipima naendelea vizuri nikarudi nyumbani kesho yake nikaenda Amana Hospitali kufanya uchunguzi tena wa uhakika hakika kweli nikafankiwa kumuona doctor nikapima vipimo vyote naendelea vizuri  nikarudi nyumbani kesho yake sikuenda popote nikampigia simu mama yangu akiwa shinyanga nikamwambia ''mama mimi nakufa nimepewa angalizo ya kufanyiwa oppression kutoa figo natakiwa kwenda India'' mama akasema mwanangu nakuja nikamwambia subiri kwanza mama nitakupa jibu kesho kweli mama akanielewa kesho ikafika asubuhi mnamo saa nne asubuhi Yule dada niliekutana nae akaja kunijulia hali wakati simjui na najua hafahamu ninapokaa na mimi sifahamu anapokaa na kubwa zaidi lililosumbua kichwa changu ni kafikaje pale nyumbani yule dada?. akamsalimia kaka maana nilikua naishi na kaka yangu na baada ya hapo akanisalimia na mimi na akamwambia kaka  ''nimekuja kumuona huyu ndugu yangu'' kaka akajua najuana nae huyu dada hakumuuliza unanakaa wapi basi Yule dada akaaga aondoke lakini kaka akamzuia akamwambia subiri tunywe chai Yule dada akawa amekataa basi kaka akamruhusu aende akasema asante kwakuja kututembelea dada akasema asanteni pia  basi Yule dada nikamsindikiza huku tunaongea na akiniambia kuwa muda wa kupona kwangu umefika, huku tukitembea na mimi nikiwa mbele  na yeye akiwa nyuma yangu maongezi yaliendelea na ghafla nikageuka nyuma na kukuta hakuna mtu yaani ni kana kwamba nilikua naongea na sauti tu bila mtu mwenyewe kuwepo nikajua labda amesahau kitu chake amekirudia nikasubiri hatokei ikabidi nirudi kwenda kumuangalia nikamuuliza kaka Yule dada yuko wapi kaka akajibu si mmeondoka wote? ndiyo tumeondoka wote nashangaa simuoni nyuma maana nilikuwa nimetangulia mbele kidogo tu  kumpeleka barabarani kwenda kupanda gari kaka akasema huyo ni mchawi ametumwa aje akumalizie wambie nyumbani kuwa amekuja mtu halafu kapotea gafla kaka anamaliza kusema hivo mara nikasikia sauti ikisema ''UMEPONA USIOGOPE'' na sauti hiyo ilikua kama mwangwi sauti ni ya Yule yule dada nikajua na kaka amesikia hiyo sauti kumbe hakusikia basi toka muda huo nikajisikia nimepona kabisa hakuna maumivu ya aina yeyote yale nikagundua Yule hakuwa mtu wa kawaida nikakaa siku tano nikaenda kumuona doctor bingwa wa figo muhimbili namshukuru MUNGU nilikuwa sisumbuliwi kuwaona madoctor kwa muda mfupi akasema mbona figo zako ziko safi hakuna tatizo nikajua kweli ile sauti ilifanya kweli uponyaji wa kweli bila kuachia makovu .Basi huo ndo ushuhuda wangu wapendwa katika BWANA YESU nawaomba tujipe moyo mtetezi yupo hata kama jaribu limeshindikanika vipi amini neno la MUNGU na jua ya kuwa BWANA YESU alikuja hata kutusaidia katika dhiki zetu na huyu dada mimi naamini alikua ni malaika aliyetumwa na MUNGU BABA ili kuleta uponyaji kwangu maana hali ilikuwa ni mbaya sana na ajabu ambayo huwa nashangaa ni jinsi alivyoniomba tujikinge wote mwamvuli na jinsi baada ya siku kadhaa alivyofika nyumbani na hatimanye alivyopotea na baadae sauti ya ushindi aliyotoa na baada ya hapo nikawa mzima na MUNGU akubariki amina.  Na hakika kuwa kwa YESU ni raha sana 

 AMOS OKELLO( MWENYE BGUO NYEKUNDU ALIYESHIKA MIC ISIYO WARELESS) AKIWA NA BAADHI YA WANAKWAYA WENZAKE WA KPC CHOIR WAKIFANYA MAZOEZI
NIKIWA NA AMOS OKELLO NJE YA KANISA LA P AG KAWE AU MAARUFU KAWE PENTECOSTAL CHURCH (KPC)
  

Comments