NAMNA PASAKA ILIVYO



Mtumishi Gasper Madumla
 
 


SOMO :NAMNA PASAKA ILIVYO.* Sehemu ya kwanza *

Haleluya…
Bwana Yesu asifiwe…

Ninakukaribisha katika mfululizo wa somo hili zuri linalokujia katika wakati sahihi.Kupitia somo hili utajifunza mambo ya msingi kuhusu PASAKA ili utakapokuwa unasherekea sikukuu hii ujue unasherekea nini.

Watu wengi wamejikuta wakisherekea pasipo kujua wanachokisherekea Au wengine ukiwauliza kwamba ;

Nini maana ya PASAKA ?

Ukweli ni kwamba utakuta hawana majibu wengine watakujibu kwamba “ Hiyo ni sikukuu tu,kama sikukuu nyingine…”

Leo ipo sababu ya kuwepo somo hili mahali hapa,Kwamba tufahamu kiundani kwa kupitia maandiko matakatifu.
Labda nianze kwa kusema kuwa ;

PASAKA ni jina la Bwana Yesu Kristo maana yeye alifanyika kuwa mwanakondoo kwa ajili ya ukombozi wako na wangu,hivyo pasaka ni jina la mwanakondoo ( 1 Korintho 5 : 7)

Neno PASAKA imetokana na neno la kiingereza ambalo ni PASSOVER/(au Easter) ( Easter Is improperly put for PASSOVER ),
Passover ni jina la sikukuu ya Wayahudi wa zamani ambalo likimaanisha Easter
{ Passover being the name of the ancient Jewish festival here referred to; while Easter}

PASSOVER,jina hili kiebrania ni PESACH, na kigiriki ni PASCHA, Tazama kwa neno hilo kwa lugha ya kigiriki linavyofanana fanana na lugha yetu ya Kiswahili.

Haleluya…

Sikia;

Ninaweza kusema kwamba ;
“ Passover, is passing over ”Kama linavyojielezea kwamba ni ile hali ya kupita kutoka sehemu moja na kuamia sehemu ya pili yenye makusudi maalumu.
Kumbuka ;
Wana wa Israeli walitoka nchini Misri kwenda mahali ambapo Bwana aliwataka waende,au watoke kwa kusudi maalumu la Kumuabudu MUNGU wa Kweli.

Tunaanza kusoma andiko hili hapa ; Kutoka 12 : 1-2
“ Bwana akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia,
Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu. ”

Mungu anazungumza na watu wake Musa na Haruni, katika nchi ya Misri. Nchi ya Misri ilikuwa ni nchi ya ugenini kwao, lakini tunaona ndipo Mungu anazungumza na watu wake akiwapa maagizo,
Tunajifunza kwamba hata katika nchi ya ugenini BWANA MUNGU anaweza kuzungumza na wewe.

Na ile kuzungumza na wewe inaonesha lipo kusudi mpaka azungumze na wewe. Musa na Haruni walikuwa Misri mahali ambapo walaambiwa watoke.
Misri ya leo yawezekana ni mahali ambapo mtu awapo kidunia au hata Misri ya leo yaweza kuwa ni katika maisha ya mapokeo ya yakufuata dini inasemaje na sio Mungu anasemaje.

Jina la BWANA libarikiwe…
Sikia;

Huko huko Misri ,Mungu akazungumza na Musa na Haruni,akawapa maagizo na agizo la kwanza anawaambia kuwa
Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwao,; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwao.
Hapa tunaona kuwa Mungu anaamua kufuta muda wao wote walioishi nchini Misri muda wa miaka mia nne na thelathini
Tunasoma ;
Kutoka 12 : 41 ;
“ Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo mia nne na thelathini, ilikuwa siku ile ile, ya kwamba majeshi yote ya Bwana yalitoka nchi ya Misri.”
Hivyo BWANA MUNGU akaanza kuhesabu kuwa mwezi huo walipokuwa wanatoka ndio uwe mwezi wa kwanza kwao.

Hii ina maanisha nini ?

Jibu :
2 Korintho 5 :17
“Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. "

Mtu akiwa ndani ya Kristo anakuwa kiumbe kipya,Katika siku hiyo ndio ilikuwa ukombozi wao wa wana wa Israel kuondoa majeshi yao na kwenda kutembea na Mungu aliye hai. Na ndio maana katika ukombozi huo,ukawafanya wawe wapya kwa kazi ya Bwana.

Yeyote aliyookoka anabadilishwa na kuwa kiumbe kipya.Nasema anabadilishwa na wala sio yeye ajibadilishe no !
Bali Hubadilishwa kwa UWEZA WA ROHO MTAKATIFU.

ITAENDELEA…

Comments