NI MAPENZI YA MUNGU TUFANIKIWE KATIKA MAMBO YOTE

 
Fahamu ni mapenzi ya Mungu wewe ufanikiwe katika mambo yako yote,Ni mapenzi ya Mungu ufanikiwe rohoni mwako na katika afya yako yote neno la Mungu linasema hivi “ Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yako yote na kuwa na afya yako,kama vile roho yako ifanikiwavyo” (3YOHANA 1:2) Yohana alimuombea Gayo maombi ya namna hiyo,fahamu hata wewe leo hii unatakiwa ujue kuwa ni mapenzi ya Mungu umuombe akufanikishe katika mambo yako yote,Fahamu hata Bwana Yesu Kristo anatufundisha sisi kuwa tunatakiwa tumuombe Mungu atupe riziki zetu zote za kila namna za siku zote, “Utupe leo riziki yetu” (MATHAYO 6:11),Watu wengi sana wanaogopa kumuomba Mungu awabariki au awafanikishe kweli-kweli, Sikia mpendwa unatakiwa umuombe Mungu akubariki sana,fahamu ni mapenzi yake akubariki tatizo liko kwako humuombi ili akupe riziki zako kila siku,watu wengi wanamuomba Mungu awape riziki zao siku za jumapili tu wanapoisema sala kuu ya Bwana!  Ukisoma maneno ya Mungu kwa makini utagundua kuwa Mungu yupo tayari kutupatia riziki zetu,ila anachokitaka ni kumuomba,sikia ikiwa wewe humuombi ili akufanikishe katika maisha yako fahamu hutafanikiwa,Yohana alilijua jambo hilo ndio maana akaamua kumuombea Gayo afanikiwe katika “mambo yake yote”. Fahamu Mungu anataka ufanikiwe katika mambo yako yote,si mpango wa Mungu ufanikiwe sehemu Fulani tu,Mungu anataka ufanikiwe katika mambo yako yote, kwahiyo ndugu unatakiwe ufahamu kuwa ni mapenzi yake Mungu umuombe akufanikishe sana katika mambo yako yote! Ngoja nikuulize unamambo gani? Muombe akufanikishe katika jambo hilo ulilonalo,sikia si mpango wa Mungu ufanikiwe katika mambo ya kiroho tu,anasema anataka ufanikiwe pia hata katika afya yako(uchumi), fahamu huwezi leo ukawa na afya nzuri ikiwa huna uchumi mzuri! Kwa maana hiyo fahamu kuwa ni mapenzi ya Mungu umuombe ili akufanikishe sana katika uchumi wako au afya yako na ya familia yako. 


Sikia maombi haya ya mtu mmoja aitwaye Yabesi,jinsi alivyo muomba Mungu na Mungu akampa alichokiomba kwani aliomba maombi hayo sawasawa na mapenzi ya Mungu. Ebu sikia “ Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze;na mamaye akamwita jina lake Yabesi,akisema,ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni,huyo Yabesiakamlingana Mungu wa Israeli akisema,lau kama kwamba ungenibarikia kwelikweli,na kunizidishia hozi yangu na mkono wako ungekuwa pamoja nami.nawe ungenilinda na maovu,ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba”(1NYA 4:9-10), Yabesi alimuomba Mungu amfanikishe kwelikweli(kiuchumi),fahamu Mungu alimpa haja ya moyo wake, sikia ni mapenzi ya Mungu umuombe ufanikiwe wewe na familia yako.pia ni mapenzi ya Mungu uwaombee wacha Mungu,ili Mungu awape afya na  baraka tele, neno la Mungu linasema hivi “ Hao makuhani wahudumu wa Bwana na walie kati ya patakatifu na madhabahu,na waseme uwaachilie watu wako,Ee Bwana,wala usiutoe urithi wako upate aibu,hata mataifa watawale juu yao;kweli waseme kati ya watu,yu wapi Mungu wao?” (YOELI 2:17) 

Neno la Mungu linamwagiza kila kuhani aseme au aombe mbele za Mungu kuwa Mungu awaondolee aibu watu wa urithi wake,fahamu katika agano jipya Mungu ametufanya watu  wote tumwaminio Yesu kuwa makuhani sikia neno lake lisemavyo“….. Kwakuwa ulichinjwa,ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wamiliki juu ya nchi” (UFU 5:9-10),Fahamu  wewe uliyenunuliwa kwa damu ya Yesu Kristo,Mungu amekufanya wewe kuwa kuhani wake. Sasa kila kuhani ameagizwa ahakikishe ana simama mbele za Mungu na kumuomba Mungu awaondolee aibu watoto wake,na moja ya aibu ambayo kuhani wewe unatakiwa umuombe Mungu aiondoe katika jamii ya watu wa muaminio Bwana Yesu ni umasikini,fahamu ikiwa wewe umokoka na ni masikini asilimia kubwa maisha yako yatakuwa ya aibu! Huta  mtukuza Mungu kwani kila mara utakuwa ni mtu wa madeni na hata watu watakuchoka kwa kuombaomba msaada,Sikia ndugu ukiwa masikini hata ndugu zako na jamaa wote wanaokuzunguka hawata kusikiliza na kukuheshimu, hata kama umeokoka,neno la Bwana linasema wazi kuwa hekima ya masikini haisikilizwi, “Ndipo nilipo sema,bora hekima kuliko nguvu;walakini hekima ya masikini hudharauliwa,wala maneno yake hayasikilizwi” (MHUBIRI 9:16), Fahamu hilo ndugu,kuwa ikiwa leo hii unataka usikilizwe katika  jamii ni lazima uhakikishe unamuomba Mungu sana akupatie mafanikio kiuchumi,fahamu kama kweli leo hii  unataka uwaambie watu maneno ya Mungu na wakae na kukusikiliza unatakiwa usiwe masikini! Ebu jiulize swali hili,ni kwanini watu wengi leo hii hawasikilizi neno la Mungu? Fahamu moja ya sababu kubwa inayosababisha watu wasisikie neno la Mungu ni umasikini uliowakalia watu wengi waliokoka! Ebu angalia mikutano ya injili jinsi inavyoandaliwa,kwa mwaka inaandaliwa mala moja,kisa ni kwa sababu ya umasikini! Ukiuliza ni kwanini mnaandaa mkutano kwa mwaka mala moja? Jibu utasikia ni kwa sababu hakuna fedha! Watu wengi waliokoka ni masikini,sasa ili waandae mkutano inabidi wachangishane wee!wadundulize wee ndipo wauandae uomkutano wa injili, mikutano mingi ya injili ikiisha viongozi huwa ni siri yao tu,kwani mara nyingi hujikuta katika teso la madeni! Kwani vijipesa vilivyokusanywa havikutosha,na ili mkutano usiahilishwe viongozi walienda kukopa kwa mtu furani,sas ukiisha mkutano viongozi badara ya kufikilia kuwalea watu waliozaliwa upya akilizao zina hamia katika suala la kulipa deni linalowakabili. 

Tufanyeje ili tutoke katika hali hii ya aibu iliyowakalia watoto wa Mungu wengi? Fahamu ni lazima uanze kuomba leo! Omba Mungu alibariki kanisa lake kwelikweli katika siku hizi,waombee watakatifu wote Mungu awape rizikizao ili wapate kumtukuza Mungu na kuipeleka injili kila kona. Fahamu watoto wa Mungu wakibarikiwa uflme wa Mungu utajengwa kwa uzuri na kwa haraka sana,na semina za kiroho zitaandaliwa mara kwa mara kwani fedha itakuwepo! Itakuwa ni rahisi sana kuwatunza watumishi wa Mungu,nao watafanya kazi kwa uzuri sana,itakuwa ni lahisi kuandaa mikutano mikubwa ya injiri mara kwa mara,na hata watu watavutiwa na maisha yako unayoishi,watatamani na
watagundua kuwa umefanikiwa kwa sababu ya Yesu,unajua watamuhitaji huyu Yesu ulie naye!Watu wengi sana wanaogopa kuokoka kwa sababu wakiwaona watu waliokoka jinsi wanavyoishi maisha ya taabu kama watoto yatima wakati wanaye Baba ambaye ni Yesu aliye sema wazi kuwa sitawaacha yatima naja kwenu, sikia ndugu ni mapenzi ya Mungu umuombe akufanikishe katika mambo yako yote,Muombe Mungu akufanikishe katika masomo yako,akufanikishe katika biashara yako,akufanikishe katika kazi zako,akufanikishe katika shamba lako akufanikishe katika familia yako Pia usiache kuliombea taifa lako ili Mungu alifanikishe sana.Sikia muombe Mungu akufanikishe rohoni na katika uchumi wako umenielewa? Basi ikiwa umenielewa anza kuomba maombi ya namna hiyo,fahamu ukiomba hivyo utakuwa unaomba sawasawa na mapenzi ya Mungu.MUNGU awabariki

Comments