NILIMPENDA MSICHANA KUMBE NI JINI NA AMENITESA SANA


Naitwa Patrick Bundala niko mailimoja Kibaha ni mwajiriwa wa serikali ni Askari ila nyumbani ni Tabora na huku niko kikazi tu, nina mke na watoto 4. Kuna kitu kibaya kilinitokea nikiwa kozi ya uongozi huko Zanzibar mwaka 2009, tukiwa kozi tulikua tunapata mapumziko siku za weekend hivyo kutumia nafasi hiyo kwenda kutembea beach na siku hiyo ya tukio baya  ilikua jumamosi ambapo tuliondoka tukiwa wengi tu kama 50 na kwenda maeneo ya kilimani karibu na migombani ambako kuna beach nzuri sana na siku ya jumamosi jioni beach huwa inajaa watu wa kila aina na siku hiyo haikua mara ya kwanza mimi kwenda huko beach kwani kila weekend lazima niende huko beach ili kuburudisha macho na kuangalia mazingira na watu maana mimi kwa Zanzibar ilikua mara ya kwanza kwenda hivyo kwa umaarufu wa Zanzibar nilitaka hadi natoka huko niwe na cha kuwasimulia huku nyumbani kumbe ilikua bahati mbaya sana kwangu siku hiyo, wakati siku hiyo tumefika beach tulitawanyika kila mtu eneo analotaka na wengine walienda kuogelea na mimi licha ya kufahamu kuogelea lakini siku hiyo sikutaka kuogelea lakini nilitaka kutafuta binti mzuri ili nimtongoze na tuwe wapenzi na nilienda pembeni kidogo eneo ambalo watu walikua wachache na kukaa mkao wa kuangalia watu na baada kama ya dakika 40 alipita dada mmoja aliyevaa ninja akiwa ni nusu mwaarabu na nusu mwafrika na nikajikuta namtamani sana alinipita kidogo na kugeuka na kuniangalia na mimi nikaona hiyo ndio nafasi ya kumwogelesha na kikamwita akaja na ajabu sikumwambia chochote lakini sijui aligundua kuwa natafuta mwanamke maana alisogea na kunisalimia na akakaa pembeni yangu na kunichangamkia sana, na kwa sababu nilitaka mpenzi nilidhani kuwa huyo ni changudoa ambaye huwa anaenda kutafuta wanaume beach, Baada ya kukaa tuliendelea na story na ajabu yule dada akaniambia mwenyewe kuwa amenipenda sana maana nimemjali na mimi nikaona kuwa  hiyo nafasi ya kumpata mrembo yule siwezi kuipoteza na muda huo huo nikaanza kumwambia mambo ya mapenzi maana nilidhani ni kahaba na nilipomwambia hivyo alicheka na kusema amekubali ila anataka ajue kwanza jina langu, kwa sababu ya kuepusha maswali ya kuulizwa zaidi na ili asije akakataa kwa sababu ya majina yangu ya kikristo japokua hata kanisani sijawahi kwenda nilimwambia kuwa mimi naitwa Saleh Juma na yeye akasema anaitwa Munira, akafurahi sana na kusema kuwa nafaa sana na amefurahi sana kukutana na mimi. Sikutaka kuopoteza nafasi hiyo nilimwambia kuwa tunaweza kuwa wote usiku ule? akasema mbona mapema sana nikasema kwa sababu amenivutia sana, akaongea kwa madaha na kusema amekubali na kwa sababu ya binti yule nilisahau yote na kumwambia tuondoke twende tukaongelee guest house akakubali na tukaondoka saa ile ilie na kupanda gari za airport na tukashukia mkunazini na kutafuta gest tulipata na nikaalipia na tukaingia chumbani na lengo langu japokua nililipia chumba hadi asubuhi lakini nilitaka tu tufanye mapenzi na niondoke kuwahi foleni ya usiku kule kozi, tukiwa chumbani tulianza michezo ya kimapenzi na akanivulisha nguo zote na mimi nikamvulisha nguo zote isipokua nguo ya ndani na baadae kidogo akashuka kitandani na kusimama huku akinitazama kwa macho makali sana nikaanza kushtuka na ghafla kibanio chake cha nywele kikaachia ghafla na tukio la ajabu sana likatokea nywele zake zikalefuka na kuongezeka zikajaa chumba chote, nikiwa nimejilaza kitandani nilikaa ghafla na baada ya muda kidogo zile nywele zilisinyaa na kuwa za kawaida na kile kibanio kijiweka mahali pake na kubana nywele, Munira akasema kuwa yeye ni jini na anataka tu damu yangu kwani ana njaa sana nilikimbilia mlangoni ghafla huku nikiwa uchi na kujaribu kufungua mlango lakini haukufunguka japokua hatukufunga, akasema siwezi kumtoroka hata siku moja na kwa sababu mimi nimempenda na yeye amependa nyama yangu na damu yangu, nilijikaza lakini nilikua hoi karibu na kuzimia na nikaona njia iliyobaki ni kupiga kele ili watu waje kunisaidia na nilipopiga kele sauti haikwenda kokote maana nilipanua mdogo kwa nguvu zangu zote lakini sauti iliyotoka ni kama namng'ong'eza mtu kiukweli nikikua kama nimechanganyikiwa na niliposhidwa zoezi hilo niliwaza kuwa njia iliyobaki ni kulibembeleza tu lile jini na nilipoliangalia nilikuta linakwato miguuni na miguu ina manyoya kama mbuzi na meno limetoa na kuwa marefu zaidi ya rula ya kupigia mistari, Hakuwa tena yule msichana mrembo munira ambaye nilimpenda sana kwa muda mfupi, Nilimwambia yule jini anibadilishie adhabu akakataa na nilijikuta naomba maombi kwa MUNGU anihurumie na ajabu kama dakika 5 zilizofuata mlango uligogwa na ghafla lile jini likawa Munira yule wa beach na kwa sababu ya mlango kuendelea kugongwa yule jini alienda kufungua na mimi muda huo nikaanza kuvaa nguo kiaskari yaani nusu dakika nimeshavaa zote, Alikua ni dada wa mapokezi akileta chakula chipsi mayai na  na soda na munira kwa ujanja akasimama katikati ya mlango na kuanza kusema sisi hatukuagiza chochote na muda huo huo nikwamwambia yule dada aingie ndani maana kuna kitu nataka kumtuma akaja na alipokaribia tu nikatoka ghafla na kumwaga kile chakula chote huku nikisema kuwa yule dada sio mtu ni jini yule dada mhudumu naye akaakimbia na sikujua kilichoendelea ila nadhani yule jini alipotea muda huohuo maana nilipofika tu nje nilimkuta akinisubiri na kuniambia sina ujanja wa kumtoroka na kwasababu ilikua ni barabarani na watu wengi wanapita nilipiga kelele na kusema jamani niokoeni na vijana fulani waliokua wanapita mmoja wao akasema wewe umekua chizi yaani unaongea peke yako niliondoka kwa kukimbia kama mita 100  na kupanda gari ambayo ilinipekeka hado kambini na nilipofika tu kambini nilimwona tena yule jini na akaniambia kuwa kuniua lazima anaiue tu tena usiku uleule nilipiga tena kele na askari wenzangu wakaanza kucheka sana wakisema nimepandisha mashetani na nikawaelezea kuwa sijapandisha chochote ila ni hali halisi na nikawasimulia mwanzo wa tukio hadi mwisho na usiku huo sikulala maana usiku wa saa 7 nilimwona tena yule munira jini na nikapiga kelele na wenzangu kwa hasira wakasema nisiwasumbue lakini mmoja wao ambaye ameokoka akaniambia namhitaji YESU ili niwe huru. Kwa sababu ya shida nilimwambia niko tayari kuokoka kuanzia sekunde ile, akasema kuwa wao wana kundi lao la maombi hapo kozi ambalo ni kundi la waliookoka kutoka makanisa mbalimbali na huwa wana ratiba ya maombi hivyo muda ukifika atanijurisha ili twende wote na muda huo akaniombea ulinzi wa MUNGU. Muda wa maombi ulipofika tulikwenda na niliombewa na wakati wa maombezi ikasikika sauti kuwa ipo siku watanipata tu. lakini namshukuru MUNGU sana maana nilipona tangu saa ile na nimeendelea na wokovu hadi leo na hakuna chochote walichofanya. Nampenda YESU na namshukuru sana kwa kuniponya na kuniokoka pia kuniepusha na mabaya yale. MUNGU akubariki sana ndugu mtumishi wa MUNGU.

Comments