Jorge
Mario Bergoglio ambaye ndiye Papa Francis I kutoka Argentina
|
Hatimae Jopo la Makardinali 115 wa Kanisa
katoliki wamemchagua Kardinali wa Buenos
Aires kutoka Latin Amerika Jorge
Mario Bergoglio (76) kuwa kiongozi
mpya atakaye chukuwa nafasi ya Papa
Benedict aliyejiuzuli hivi karibuni.Papa Mpya alichaguliwa katika duru ya tano ya upigaji kura uliofanywa na
makadinali 115 waliokuwa wakikutana katika kanisa la Sistine Chapel
huko Vatican , Roma.
Jorge Mario Bergoglio
ambaye ni Muagrgentina tayari amechagua jina la atakalo litumia katikakipindi
chake cha Uongozi kuwa atatambulika kama Papa Francis I.
Jopo
la Makardinali wamemchagua Cardinali kutoka Latin America Cardinal Jorge Mario Bergoglio, kushika wadhifa mpya wa Papa katika uchaguzi uliofanyika kwa mara ya
tano kwa kura zilizopugwa na Makadinali 115 waliokuwa wakikutana katika kanisa
la Sistine Chapel huko Vatican , Roma.
Comments