Posted by
Peter Mabula
- Get link
- X
- Other Apps
Mtumishi Gasper Madumla |
SOMO :PENDO LA MUNGU KWETU.
Haleluya…
Jina la BWANA MUNGU LIPEWE SIFA...
Karibu mpendwa nikushirikishe tafakari hii fupi ya leo kuhusu pendo la
Mungu katika maisha yetu.Kwanza kabisa napenda ifahamike kwamba Mungu
wetu atupenda kiasi ambacho hakuna yeyote atakaeweza kueleza namna Pendo
la MUNGU kwetu lilivyo,
Lakini ninachoweza kusema kwako ni
kwamba Yeye Bwana Mungu ni PENDO.Hivyo upendo wake kwetu sisi ni upendo
usio na mwisho,( Endless love).Mungu ameachilia upendo huu kwetu sote ,
yaani kwa wale wacha-Mungu wake, hata kwa wale wasio wacha-Mungu,akitoa
Fursa ya pekee kwa wale ambao sio wacha-Mungu kwamba labda ipo siku
moja wataokoka nao watakuwa mali yake kweli kweli.
Tazama kama
ni jua sote twapata,au kama mvua sisi sote twapata,Labda kama ingekuwa
yeye Bwana Mungu ni mbaguzi katika Pendo lake,Basi ni dhahili kabisa
kama ingekuwa ni mvua angewanyeshea kundi la watu Fulani kisha wengine
awanyimwe.
Labda pata picha hii ;
Tuseme kwamba ndio waovu
wote wapo Dar huko Mbezi.Na wema wote wapo Dar huko Magomeni.Kisha
mvua ikawanyeshea watu wa Magomeni na watu wa Mbezi wasipate mvua,
Una fikiri ingekuwaje ?
Haleluya…
Lakini Mungu wetu sio wa kiivyo. Tazama mfano wa NGANO na MAGUGU.
Biblia inatueleza mfano mzuri sana hapa,Kwamba bwana shamba alipanda
mbegu njema katika Konde lake/katika shamba lake,
Baadae adui akaja akapanda MAGUGU.Kisha wale watumwa wake wakamuendea kumpasha habari ;
Tunasoma Mathayo 13 : 27-30
“ Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu?
Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye?
Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing'oa ngano pamoja nayo.
Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno
nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita
mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu. ”
Bwana wao
alipotambua kwamba MAGUGU yamepandwa na adui katika shamba alilopanda
NGANO akasema viache vikue kwa pamoja hadi mwisho,
hii
inamaanisha kwamba kama suala la kupata maji,au samadi,au kupaliliwa
katika shamba hilo,basi NGANO na MGUGU vilikuwa vinapata vyote kwa
pamoja pasipo kubaguliwa,
Lakini hapo kuna mtego kwamba mwisho
katika mavuno, ndipo zitatengwa NGANO na MAGUGU,Hapo ndipo MAGUGU
yatafungwa na kuchomwa moto,Bali NGANO itakusanywa na kutunzwa.
Sawa sawa na watu wote tuliopo chini ya mbingu hili,Kwamba tumeachwa tuendelee na mambo yetu mpaka mwisho.
Yaani wale wenye kuokoka wataendelea na wale wanaokataa au wale waovu
wote nao wataendelea na mambo yao,Lakini hapo mwisho ndipo kutakuwa na
kilio na kusaga meno kwa wale wasiomtaka Mungu sasa.
Wakikataa
kabizi maisha yao kwa Bwana Yesu awe Bwana na Mwokozi wao,wakidhani
kwamba wanafanya mambo yao kwa akili zao wenyewe,KUMBE WAMESAHAU MTEGO
KWAMBA MWISHO KUTAKUWAKO NA KILIO NA KUSAGA MENO.
Ili umpende Mungu ni lazima ufahamu namna ya pendo lake kwako,kwamba ujue Yeye alikupenda kwanza (1 Yoh 4 :19).
Tazama bahari ,ambayo mwanzo wake unaweza kuuona lakini huwezi kuona
mwisho wake,Huo ni mfano mdogo wa UPENDO wa Mungu kwetu sisi,Tena siwezi
kuufananisha na upendo wa Mungu kwetu,maana upendo wa Mungu kwetu
hauelezeki.
Ukijua kwamba Mungu anakupenda sana kiasi kwamba hataki upotee maana amekupa nafasi tena labda utajerea kwake kwa TOBA.
Maana anasema “ Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.
Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako. ” Isaya 43 : 25-26
• Watu wengi siku ya leo hatupendani,kwa sababu tumemuacha Mungu kwa kusahau au kutokujua UPENDO wa Mungu kwetu.
• Ukiona mafarakano katika familia ujue kiwango cha kumpenda Bwana
Mungu kiko chini sana au kiwango hicho hakipo kabisa,Maana yeyote
ampendaye Mungu,atampenda na jirani yake.
Biblia inatutaka tupendane maana tukisema tunampenda Mungu kisha tunawachukia majirani zetu tutakuwa waongo( 1 Yoh.4: 20)
Hivyo wito wangu kwako ni kuomba Neema ya kukaa katika pendo la
Mungu,Nafasi ndio sasa ya kuifanyia kazi.Waweza kufanya toba kwanza na
kisha omba neema hii.
UBARIKIWE. BY MTUMISHI GASPER MADUMLA
- Get link
- X
- Other Apps
Comments