TABIA ZA MUME ASIYETAMANIKA

Pastor Donis and Nnunu Nkone
NDOA - TABIA ZA MUME ASIYETAMANIKA !
1. Ni MBISHI na ana HASIRA KWELI - anabishana na mke mpaka anajisahau,
2. Ana tabia ya uchoyo, ubinafsi, hana moyo wa huruma kwa mke wake,
3. Ni mbania pesa saaaana isipokua tu kwa mama yake mzazi tu ndio pesa inatoka,
4. Hataki mke ajue kiasi cha pesa au mshahara wake wote,
Basi Ndoa yenye Mume wa namna hii INAHITAJI MAOMBI YA MNYORORO !
NDOA - TABIA ZA MKE ASIYETAMANIKA !
1. Ana tabia ya uchoyo, ubinafsi, hana moyo wa huruma kwa Mume,
2. Kwa kuwa ana kazi na mshahara mkubwa kuliko mume, basi hamuheshimu mume kama inavyotakiwa,
3. Ana HASIRA na akikasirika, penzi linawekwa KUFULI YA MJERUMANI,
Basi Ndoa yenye Mke wa namna hii INAHITAJI MAOMBI YA MNYORORO !
Pastor Nnunu alisema "NDOA NI HUDUMA, ITUNZE KWA MAOMBI".
Pastor Donis and Nnunu Nkone, Senior Pastors of All Nations BreakThrough Church - Gahanna Ohio.
FROM OUR NEW BOOK COMING UP SOON !

Comments