EPUKA ULAJI WA SUKARI NYINGI


Mtumishi Gasper Madumla


Kama kuna kitu kinapendawa sana na watu wengi ni sukari, lakini siyo nzuri kwa afya yetu inapotumiwa kupita kiwango. Kiwango cha kawaida cha sukari kinachoruhusiwa kutumiwa ni kijiko kimoja kidogo (teaspoon),

kinapozidi hapo huwa kinachangia kudhoofisha mfumo wa kinga ya mwili. Inaelezwa kuwa chupa moja ya soda ina karibu vijiko 6 vya sukari. Hivyo kama wewe ni mnywaji mkubwa wa soda na vinywaji vingine vya aina hiyo, utaona ni kiasi gani unaharibu kinga yako ya mwili kadri unavyotumia kila siku!

Mpendwa punguza sana unywaji wa soda au vitu vyenye sukari sana Sio vizuri kwa afya yako
UBARIKIWE. By GASPER MADUMLA

Comments