Posted by
Peter Mabula
- Get link
- X
- Other Apps
![]() |
Vicent Mwengo |
HATARI YA MAISHA.
KUONGEZEKA NA KUYATUMAINIA MAARIFA YA KIDUNIA.
Kwa maana rahisi ya neno maarifa au hekima ni ufahamu/uwezo wa kutambua
jambo na kukabiliana na jambo hilo. Ninapozungumzia habari za hekima au
maarifa ni namna watu wanavyokabiliana na maisha, lakini sasa shughuli
zako za kila siku ndizo zinakufanya usiweze kuzikumbuka habari za Mungu?
Liko tatizo la watu kumsahau Mungu kwa sababu ya shughuli zao cha
kiuchumi, watu kujiongezea na kujivuna mali zao ambazo wanaamini ndio
msaada wao maishani lakini wanasahau kama uhai walionao ni neema tu.
Watu ambao wamekuwa na elimu ya darasani ndio wamekuwa na mioyo migumu
tangu enzi za Yesu lakini kwa kipindi hichi tatizo hili limeongezeka kwa
kasi, watu wanajivunia elimu zao; fanya uchunguzi utagundua wasomi ndio
wanaoongoza kwa zinaa, dhuluma, uongo,
wizi na mengine mengi yaliyo maovu. Naomba ujiulize mimi na wewe tuko
kwenye kundi lipi. Nikwambie tu hivi; hapana!! Tusikubali, pamoja na
mambo yote tumtangulize Mungu. Jifunze kupitia hadithi chache toka
kwenye kitabu kitakatifu.
Luka 12:13-21
Mathaayo 6:19-21
Muhubiri 6:1-7 kaa chini zisome kwa makini utaelewa.
NB: MKUMBUKE MUNGU, MHESHIMU MUNGU KWA KUTEKELEZA MAAGIZO YAKE. (soma Biblia utayakuta maagizo).MUNGU akubariki sana by Vicent Mwengo
- Get link
- X
- Other Apps
Comments