HEKIMA YA MUNGU





“Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu ;ila si hekima ya dunia hii,wala ya hao wanaoitawala dunia hii,wanaobatilika;bali twanena hekima ya Mungu katika siri,ile hekima iliyofichwa ,ambayo Mungu aliazimu tangu milele,kwa utukufu wetu;ambayo waitawalayo dunia hii hawaijui hata mmoja;maana kama wangaliijua[Yesu] ,wasingalimsulubisha Bwana wa utukufu ;” 1wakorintho 2:6-8
Hekima hii ya MUNGU ni YESU,ambapo kwa wafalme na watawala wa dunia hii wamefichwa,ndiyo maana hawamwamini,hawajampokea kama Bwana na mwokozi wao,wamemkataa katika fahamu zao,na wala hawaamini kuokoka.Yesu ni hekima ya MUNGU,unapo mpokea ndipo unapopata ufunuo wote wa kimungu ndani yako na ndipo unapopata kumjua Mungu baba na urithi katika ufalme wa milele,na bila Yesu hakuna uzima wa milele,hakuna kuingia mbinguni.
Hekima hii ya MUNGU ndiyo inayofanya kazi ndani yetu tumwaminio na ni hekima ambayo ulimwengu huu hauwezi kushindana nayo maana imepita fahamu za wanadamu,Mungu anatukuzwa katika hiyo na matumaini ya waadamu yanarejeshwa upya ndani yake. “Enenda pamoja na wenye hekima nawe utakuwa na hekima;Bali rafiki wa wapumbavu ataumia”Mithali 13:20. Hekima sahihi iko kwa YESU KRISTO hivyo ni heri kila mmoja wetu akamchagua BWANA YESU ili hekima ya kimungu ifanye kazi ndani yake. MUNGU BABA wa mbinguni akubariki sana

Comments