Posted by
Peter Mabula
- Get link
- X
- Other Apps

BWANA YESU APEWE SIFA…
Wapendwa wa Mungu nami niwaletee maneno ya MUNGU.
Kwenye maisha ya kawaida ya mtu yeyote kitu ambacho humfanya ajisikie
furaha sana ni uhuru wa mawazo na matendo, kwa hayo huamini nafsi yake
imeridhika kwayo.
Katika uhuru huo mtu anakuwa anawaza pia hasa
matendo ambayo ndiyo huonekana kwa wanadamu huyatenda pia. Mtu huyo
huyatenda na huwa haijalishi kama yanawaudhi wengine au hapana lakini
ili mradi huufurahisha moyo wake basi huyatenda tu. Uhuru huu mtu huwa
nao tu kwa sababu hakuna jambo au mtu yeyote ambaye anaweza kuingilia au
kuupunguza uhuru huo. Cha ajabu ni kwamba upo wakati uhuru kwa mtu
hubadilika, hupungua na kuanza kufanya kwa misingi ya mamlaka nje ya
kichwa au mawazo yake. Ni wakati huu ambapo mtu hupata shida kwa sababu
amebadilishiwa utaratibu wake wa kuishi iwe kwa kutaka au kulazimishwa
lakini baada ya muda huwa ni maisha yake ya kawaida kwani huyazoea.
Fikiria mtu anapokuwa chini ya mamlaka fulani hususani za utumishi (kuwa
chini ya bosi). Yako mambo ambayo kwa mazoea yako ulikuwa unayatenda
kwani ulikuwa ni uhuru wako lakini kwa sababu sasa uko chini ya mamlaka
ya mtu huyaachakuyatenda kwani mamlaka hayo haiyapendi au ina utaratibu
wake. Fikiria ulikuwa umezoea kuvaa viatu vya wazi/sandles na pensi,
baadhi ya misuko kwa wadada, nguo fupi na zinazoonesha maungo ya ndani
lakini ukifika kwa bosi anakwambia style hiyo hatuitaki vaa hivi na
uonekane hivi la sivyo huna kazi. Kwasababu ya kuhitaji kazi mtu huyo
hubadilika na kufuata utaratibu huo wa kazini na kuacha maisha yake ya
kawaida,
Pia yamkini kwa sababu mtu huyo alizoea kuamka saa
tatu pindi hana kazi baada ya kupata kazi hulazimika kuamka saa 12 au
saa 1 ili kuwahi kazini aendane na masharti na taratibu za kazi.(hiyo ni
baadhi ya mifano tu) katika maisha ya kimwili ya kila siku.
Vivyo hivyo maisha ya kimungu yana sheria taratibu, na masharti yake
pia. Unapoanza maisha ya kimungu ni lazima yako matendo na mwenendo wa
fikra zako kubadilika pia. Mpaka unamtafuta mungu maana yake umetambua
dhambi za maisha yako ndio maana ukazikimbia, mmhh haiishii hapo,
inapasa kukimbiambali zaidi ktk na kuyaacha mazoea yako ili kishi maisha
yenye msingi wa kimungu na kumpendeza mungu na watu pia. Tunapoamua
kumtumikia bosi wetu mungu ambapo malipo yetu ni kufika mbinguni ni
lazima tuache baadhi ya mazoea yetu mabaya. (flp 1:27)
Soma filp 3;1-10
Nizingatie filp 3:7 lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya kristo.
Hapa Paulo alikuwa akiwahadithia wafilipi habari za nyakati zake kabla
ya kumpokea kristo kwamba aliyatenda kwani yaliufurahisha moyo wake, lkn
baada ya kumpokea kristo sasa anachukua gharama ya kuyaacha.
Katika mengi unayoyajua kwa uzoefu wako wa maisha mimi nitazungumzia jambo moja tu
MAVAZI.
Suala la mavazi sijui kama watu huwa wanalizingatia hussani wale wenye
jukumu la kuhubiri au kufundisha neon la Mungu. Elewa vizuri dhana hii,
“Mungu anaangalia moyo wako lakini wanadamu wanaangalia matendo yako,
wakiyaona mazuri huamini lakini wakiyaona mabaya hawana haja na Mungu
wako”
Angalia habari hizi, watu Fulani wakajisemea; aaahh kwa jinsi alivyo huyu hata mimi leo nikiokoka siwezi kuvaa hivi.
Mahala Fulani watu wakishuhudiwa ibada ya nyumba kwa nyumba walisema;
aaa aaahhhh azungumze huyu lkn huyu sisi hatutaki atushuhudie kwani naye
anahitaji kushuhudiwa (mavazi yake yalikuwa mabaya)
Mhubiri
akihubiri na hereni zake ndefu sana na madoido mengi, mshirika mmoja
akaulizwa umeelewa somo la leo? Alichosema aah hivi zile herein zinauzwa
shilingi ngapi? Na zinapatikana wapi kwani makubwa!!!
Mhubiri
mmoja akiwa madhabahuni akidhani watu walikuwa wanasikiliza neon kwa
makini kumbe watu walikuwa wanatafakari hivi kile kikofia alichovaa
kinauzwa shilingi ngapi kwani kina mbwembwe kwelikweli.
(hiyo ni baadhi ya matukio niliyowahi kupata kuyasikia au kuyaona kwenye huduma mbalimbali)
Haijalishi kama wewe ni muhubiri, mwalimu au muumini wa kawaida je
unajiwekaje kimavazi mpaka wengine waseme hakika huyu amebadilika.
MWISHO NIMALIZIE,
TAFAKARI, JIPIME MWENYEWE KAMA MTU WA MUNGU NA MAISHA YAKO YAWAFUNDISHE WENGINE.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments